Sunday, 18 October 2015

DKT BILALI AWEKA JIWA LA MSINGI MRADI WA VITUO VYA MAPUMZIKO KWA WASAFIRI NCHINI

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Generali Raphael Muhuga  kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Davis Mwamuyange akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi mbela ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. Mradi huo unatekelezwa na Mufindi Environmental Trust (MUET) kwa kushirikiana JKT. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali  akiwaaga wananchi wa Kijiji cha Idetero baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF) mstaafu Generali Robert Mboma ambaye pia ni mlezi taasisi ya Mufindi Environmental Trust (MUET) akitoa hotuba mbele ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali  wakati wa kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana.

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali  akipeana mkono na Mwenyekiti Mtendaji wa MUET, Godfrey Mosha (kulia) baada ya kukabidhiwa taarifa ya ujenzi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana.  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Generali Raphael Muhuga jana.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akiongea na wananchi wa Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa.

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akisalimia na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa alipowasili uwanja wa ndege wa Nduli jana kabla ya kwenda kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana.

Mwenyekiti Mtendaji wa MUET, Godfrey Mosha akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo.




Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Idetero akifuatilia hafla hiyo (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...