Sunday, 18 October 2015

KUJISAIDIA PORINI KWA WASAFIRI SASA BASI...!

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akikagua ujenzi wa mradi.

Dkt Mohamed Gharib Bilali (Picha na Friday Simbaya)

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali amesema tabia ya kujisaidia porini kwa wasafiri kama wanyama kwa lugha maarufu ya “kuchimba dawa,” sasa basi, baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini.

Alisema kuwa kwa muda mrefu abiria wanaosafiri katika barabara kuu, wamekuwa wakipata taabu pindi wanapohitaji sehemu za faragha.

Dkt Bilali alisema hayo katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana.

Mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini unakusudia kujenga vituo vya mapumziko kwa wasafiri 44 nchi nzima katika barabara kuu zote nchini.

“Jambo hili limefikia katika hatua mbaya hata kukiuka ustaarabu wa binadamu kwa kujisaidia porini kama wanayama. Tabia hii si ya ustaarabu inadhalilisha utu wetu…,” alielezia Dkt Bilali.

Alisema kuwa katika karne ya leo si ya kuendelea “kuchimba dawa” na kuipongeza taassi ya Mufindi Environmental Trust (MUET) kwa kushirikiana JKT kubuni mradi wa kujenga vituo vya mapunziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini.

Aliongeza kuwa hatua ya MUET kubuni jambo hili inastahili pongezi na kuungwa mkono na wadau wote ili kuhakikisha malengo yake yantimia kwa kujenga vituo hivyo.

Shirika la MUET tangu kuanzishwa kwake, limefanya mambo mengi, ikiwa ni pamoja na; kuhamasisha upandaji miti kwa watu binafsi, kampuni, taasis za dini na serikali, kuboresha vyanzo vya maji, kutoa elimu ya kuzuia uchomaji misitu na kutoa elimu juu ya ugonjwa wa UKIMWI.

Aidha, Dkt. Bilali alisema kuwa ili kujenga nchi yetu,tunahitaji watu wenye afya bora. Moja ya mambo muhimu katika kuboresha afya za watu ni suala zima la usafi pamoja na kutunza mazingira kwa ujumla.

Alisema kuwa hatuwezi kuzungumzia usafi katika mazingira tunayoishi bila kutaja suala la vyoo.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya nne na zilizotangulia, imefanya jitihada kubwa kuimarisha sekta ya miundombinu ya barabara nchini ambapo karibu mikoa yote nchini imeunganishwa kwa barabara ya lami.

“Natoa rai kwa wadau na mashirika mbalimbali nchini kuiga jambo jili jema na kusaidia shughuli hii muhimu. Barabara za nchi yetu ni nyingi na maeneo ni mapana, hivyo kwa taasis moja peke yake kufanya jambo hili ni kazi ngumu,” alisema Dkt. Bilali.

Aidha, aliwashukuru pia wadau mbalimbali waliojitokeza kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa vituo vya mapumziko na vyoo. 

Wadau hao ni pamoja na serikali ya china, jeshi la wananchi wa Tanzania, kumpuni ya simu za mikononi ya Airtel, Mustafa Sabodo, Mufindi Tea Companya, MUCOBA Bank, PSPF na TANESCO.

Wakati huohuo, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali aliwakumbusha watanzania wote kwamba oktoba 25 mwaka huu ni siku muhimu katika historia ya taifa.

Alisema kuwa ni siku ambayo tunaenda kupiga kura ya kuchgua viongozi katika ngazi mbalimbali.

Alitoa wito kwa watanzania wote kujitikeza kwa wengi na kutumia haki yao ya kidemeokrasia kwa kuchagua viongozi wanaowapenda.

“Tukumbe kwamba viongozi tutakaowachagua ndio watakuwa dira ya nchi yetu katika kipindi cha miaka mitano ijayo,” alisema Dkt Bilali.



mwisho

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...