Katika hali ambayo haikutarajiwa Mwenyekiti wa TLP taifa, Augustino Mrema jana amemnadi mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli kuwa ndiye anafaa kuwa Rais wakati chama chake kikiwa kimemsimamisha, Macmillian Lyimo kuwania nafasi hiyo ya Urais kwa tiketi ya TLP.
Hali hiyo ilianza kwa Dk Magufuli kumpigia debe Mrema anayewania ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP kwa kusema kuwa ana historia nzuri na uzoefu katika uongozi kuliko wengine.
Dk Magufuli alisema hayo jana wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa polisi Himo ambapo alisema wananchi wasikosee kwenye kupiga kura na kuwa hatakama hawaitaki CCM, basi wampigie kura Mrema.
No comments:
Post a Comment