Friday, 9 October 2015

MARAIS WASTAAFU KUTOKA AFRIKA WAJA KUONGOZA UFUATILIAJI WA UCHAGUZI...



Marais wastaafu wawili kutoka Afrika, watakuwa miongoni mwa waangalizi wa kimataifa watakao kuepo Nchini kuangalia Jinsi Uchaguzi mkuu utakavyo endeshwa Tarehe 25 Oktoba.

Hawa ni Rais mstaafu Goodluck Jonathan wa Nigeria ambaye ataongoza timu ya waangalizi upande wa Jumuia ya Madola na kiongozi wa zamani wa Mozambique Armando Guebuza ambaye ataiongoza timu ya waangaliaji upande wa Umoja wa Afrika.

Ujio wao ulibainishwa jana,wakati wizara ya mambo nje,ushirikiano wa kimataifa na umoja wa mataifa walipo toa taarifa kwenye vyombo vya habari ku washiria miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

Timu za Jumuia ya madola na Umoja wa Afrika watakuwa miongoni wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25,waangalizi wengine ni kutoka Jumui ya Ulaya na SADC.

Huu ni uchaguzi Mkuu wenye wafuatiliaji wengi kutoka Nchi za nje.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...