Jaji Mstaafu Damiani Lubuva
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi kutoruhusu vikundi vya watu karibu na vituo vya kupiga kura kwa madai ya kulinda kura.
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa mkutano wa tume na wasimamizi wa uchaguzi wakiwemo makamanda wa polisi wa mikoa nchini.
Jaji Lubuva ameeleza lengo la mkutano huo uliofanyika jana, ni kujadili na kupeana uzoefu juu ya wajibu na taratibu za mchakato wa uchaguzi kuanzia sasa mpaka hapo muda wa kutangaza matokeo.
Pamoja na hayo kiongozi huyo wa NEC amewataka washiriki wa kikao hicho kuzingaia maadili na kusimamia makubaliano yatakaofikiwa katika mkutano huo.
Zimebaki siku 16 kufikia uchaguzi mkuu mwaka huu na tayari tume ya uchaguzi imeshakutana na makundi mbalimbali ya wananchi kuelezea maendeleo na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na tume hiyo katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unamalizika kwa amani.
No comments:
Post a Comment