Friday, 16 October 2015

Williamu lukuvi amembeza mpinzani wake katika jimbo la ismani

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi

Na fredy mgunda, Ismani
 
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi amembeza mgombea mwenzake anayegombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Patrick Olle Sosopi na kusema kuwa Sosopi hata afanye hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kauli ya Lukuvi aliitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Igingilanyi,Kising’a,Kinywang’anga,Mkungugu,Matembo na Ilambilole vilivyopo tarafa ya Isimani katika Jimo la Ismani alisema kuwa Sosopi hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa maana hana staha ya kuweza kuwashawishi wananchi kuwaletea maendeleo na badala yake anawabeza wagombea wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa kusema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 ya ubunge wa Lukuvi hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na chama hicho.


“Mimi kiatu change navaa namba nane Sosopi anavaa namba moja hivi kweli ataweza kuwa mbunge wa jimbo hili?alihoji huku akishangiliwa sana na wananchi hao,kiukweli niwaambie kama mnataka maendeleo kichagueni CCM ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo na sio chama kingine.”alisema Lukuvi


Akiwa katika kijiji cha Kinywang’anga Lukuvi aliahidi kuwatafutia wananchi hao madaktari wa kutosha kwenye zahanati zilizopo kwenye jimbo hilo pamoja na dawa za kutosha ili kuendeleza huduma nzuri ya afya kwenye jimbo lake.


Alisma kuwa akatika kuendeleza kuduma nzuri ya afya tayari ameagiza gari ya kubebea wagonjwa(Ambulance) nchini Japani yenye gharama ya Tsh.mil 120 kwa ajili ya zahanati ya kijiji cha Kinywang’anga.


Alisema kuwa kwa sasa tayari ujenziwa zahanati ya kisinga unaendelea na wanajenga wodi ya watoto,wodi ya wazazi pamoja na nyumba za kuishi watumishi ikiwa maendeleo yote yameletwa chini ya uongozi wa CCM.


Alisema kwa kipindi cha miaka miatano ijayo atahakikisha wananchi wake wanapata maji ya uhakika kutoka Jimbo la Iringa mjini ambayo yanatokana na Mto wa Ruaha.


“ Tayari fedha za kuvuta maji yam to Ruaha kutoka Iringa mjini hadi Ismani tumeshapata,wataalamu tayari wapo na wamesema muda wowote kuanzia sasa zoezi la maji Ismani litaanza”alisema Lukuvi


Aliongeza kuwa uongozi wa serikali ya magufuli hata kabla ya kuamua kugombea Urais tayari alishaweka mpango wa kutengeneza barabara ya Kising’a,Ilambilole,Mikongwi,Ngano hadi Ismani tarafani kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km.35 kwa gharama ya zaidi ya Uro milioni tano ambapo tayari ujenzi huo umeshaanza.


Wakati akihutubia wananchiwa kijiji cha mkungugu alisema kuwa atahakikisha atapandisha kiwango cha elimu kwenye jimbo hilo pamoja na kuweka haki sawa kwa wanawake na wanaume katika kumiliki ardhi.


Hata hivyo alisema kuwa suala la umeme kwenye jimbo hilo kwa baadhi ya maeneo ni la muhimu kwa sababu kuna maeneo yaliyopo ndani ndani hayana umeme hivyo atahakikisha ataleta nguzo kwa haraka ili wananchi hao waweze kuwa umeme.
 
“Nitawapigania kuhakikisha umeme unaingia kwenye vijiji vilivyojificha sana ndani ndani na nawaambia lazima nitawaletea nguzo kwa maana mimi mwenyewe jambo la nguzo sitoshindwa,”alisema Lukuvi.
 
Hata hivyo aliwataka wananchi hao kumchagua mgombea urais wa CCM John Magufuli,mgombea ubunge Williamu Lukuvi pamoja na mgombea udiwani wa kata ya kising’a Ritta Malagala ili waweze kuwaletea maendeleo ya jimbo hilo na sio mtu mwingine.
 
Alisema kuwa kwa uongozi wa Magufuli yeye hataki mchezo huu ni wakati wa kazi na sio lelemama na kama kutakuwa na kiongozi ambaye ataonesha amekaa legelege lazima atanyooka kwa maana magufuli hapendi mtu ambae sio mchapa kazi.




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...