Thursday, 19 November 2015

Kampuni ya TTCL Yakisaidia Vifaa Tiba Kituo cha Afya Buguruni Dar


Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imetoa msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia) ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia) ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa tatu kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada katika kituo cha afya cha Buguruni leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea na kushoto kwake ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.

KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imekitembelea kituo cha Afya cha Buguruni cha jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa pamoja na dawa kwa ajili ya kukiwezesha kutimiza majukumu yake ya kuwahudumiwa wagonjwa mbalimbali wanaokitegemea kituo hicho.

Katika zoezi hilo, TTCL imekabidhi mashuka 100, Vyandarua 100, Maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho kwa ajili ya kuwahudumiwa wakazi wa maeneo hayo kiafya.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemas Mushi alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa kampuni hiyo katika kurejesha faida kwa wananchi ambao ni wateja wa kampuni hiyo. Alisema wanaamini msaada huo unaenda kuwahudumia wananchi ambao ndiyo wateja wa kuu wa huduma za TTCL.

"...Vifaa hivi vinakwenda kuwatibu wananchi ambao tunaamini ni wateja wetu, hivyo wakiwa na afya njema ndiyo furaha kwetu na kuendelea kushirikiana nao kihuduma. Huu ni utaratibu wetu wa kawaida kila tunapopata kidogo tunakirudisha kwa wananchi...leo tumetoa mashine, mashuka 100, vyandarua 100 na dawa ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwa wateja wetu," alisema Meneja huyo wa TTCL.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...