Thursday, 19 November 2015

KASSIM MAJALIWA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU SERIKALI YA AWAMU YA TANO




Na Khalfan Said
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hatimaye ametungua kitendawili cha nani atakayekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kumteua Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi,  Kassim Majaliwa.

Spika wa Bunge Job Ndugai, alipokea bahasha yenye jina la mteule huyo wa Rais, kutoka kwa Mpambe wa Rais, ambaye akiwa ndani ya sare zake za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, aliongozwa na wapambe wa Bunge hadi kwenye meza ya Spika Ndugai na kumkabidhi bahasha hiyo mapema  Novemba 19, 2015.

Baada ya Mh. Ndugai kupokea bahasha hiyo aliwaonyesha wabunge na kusema bahasha hii imewekewa seal, hivyo akamwita Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila na kumtaka aifungue ili kujua jina la Waziri Mkuu ni nani.

Dkt. Kashilila aliifungua bahasha hiyo na kukumbana na bahasha ya pili, hata alipoifungua bahasha hiyo ya pili akakumbana na bahasha ya tatu na ilipofungunliwa akakutana na kadi maalum yenye ujumbe ulioandikwa kwa mkono na Mh. Rais mwenyewe kuonyesha kuwa haikupitia kwenye mkono wa mtu mwingine na hivyo kusoma jina la mteule huyo ambaye sasa anasubiri kuthibitishwa na wabunge baadaye Alhamisi Novemba 19, 2015 kwenye kipindi cha bunge majira ya jioni

Kassim Majaliwa alikuwa Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), kwenye serikali ya awamu ya nne akishughulika sana na masuala ya elimu.

Kassim Majaliwa alizaliwa Desemba 22, 1960 huko mkoani Lindi, na amekuwa mbunge wa jimbo ;la Ruangwa moani Lindi tangu mwaka 2010.

Chini ni matukio mbalimbali ya kiutendaji ambayo Kassim Majaliwa alikuwa akiyatekeleza kwenye nafasi yake ya Ubunge na Unaibu Waziri wa TAMISEMI






No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...