Tuesday, 16 February 2016

Tigo yafungua duka Jipya mjini Tunduma



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akizungumza na wakazi wa Tunduma na wafanyakazi wa duka jipya la Tigo Tunduma katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita 




Mkuu wa wilaya ya Momba, Richard Mbeho, akiongea na wakaazi wa Tunduma (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa duka jipya la Tigo lilipo mjini Tunduma, Mkoa wa Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita 





Wakazi wa Tunduma na wafanyakazi wa Tigo wa duka jipya la Tunduma wakisiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Momba, Richard Mbeho,(hayupo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo mwishoni mwa wiki iliyopita . 





Mkuu wa Wilaya ya Momba, Richard Mbeho, aliyeko kulia na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, Meneja Ubora na Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola,Meneja wa Operesheni kwa wateja Tigo kanda ya kusini, Laverty Khana(Kulia), wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa duka jipya la Tigo lililopomjini Tunduma mwishoni mwa wiki iliyopita 



Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Momba, Richard Mbeho, na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga,wakimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Tigo wa duka la Tunduma kuhusu huduma zitakazotolewa katika duka hilo lililofunguliwa mwisho mwa wiki iliyopita. 





Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga na Meneja wa Operesheni kwa wateja Tigo kanda ya kusini, Laverty Khana, wakimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Momba, Richard Mbeho aliyehudhuria hafla hiyo kama mgeni rasmi 





Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Tigo wa duka jipya la Tigo Tunduma mara baada ya ufunguzi wa duka hilo 

Kampuni ya simu ya Tigo imefungua duka jipya Tunduma ambalo limepunguza adha kwa wateja wa kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya kusini Bw.Jackson Kiswaga alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.

"Kampuni ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika eneo la Tunduma ambapo kwa pamoja tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa kutumia simu za mkononi"Alisema Kiswaga. 

Kiswaga alisema kuwa duka hilo linategemea kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za simu na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.

Kwa upande wa katibu wa
mkuu wa wilaya ya Tunduma Mhe. Richard Mbeho alipongeza hatua za Tigo za
ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa
wilaya ya Tunduma. 









No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...