Tuesday, 16 February 2016

Tigo yatahadharisha wateja dhidi ya matumizi ya simu bandia



Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zakaria akielezea athari za matumizi ya simu bandia kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika mapema leo katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha 

Dar es Salaam, Februari 16 2016 - Watumiaji wa simu za mkononi wameonywa dhidi ya matumizi ya simu bandia na zisisokidhi viwango vya ubora ambazo tayari zimetangwa kupigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Kutokana na sababu hiyo, Tigo, ambayo ni kampuni ya kidijitali, imeanza kuendesha kampeni ya kuhamasisisha wateja wake na umma kwa jumla kupitia vyombo vya Habari inayolenga kuwaepusha na athari za matumizi ya simu bandia.

``Kwa mujibu wa maelekezo ya TCRA matumizi ya simu za mkononi ambazo namba zake za utambulisho wa kimataifa (IMEI) ni bandia yatapigwa marufuku kutumika kwa mitandao yote ya simu nchini Tanzania kuanzia Juni 16 mwaka huu. Ili kujiepusha na usumbufu wowote utakaotokana na hatua hii tunawashauri wateja wetu kujipatia simu halisi na bora kutoka maduka ya Tigo yaliyo karibu nao,`` alisema Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zakaria.

Ripoti ya utafiti ulichapishwa katika tovuti ya GSMA ("http://www.gsma.com" www.gsma.com ) inasema kwamba tofauti na ilivyo kwa simu halali ambazo hupitia mamia ya hatua mbalimbali za kuhakiki ubora wake kabla ya kupelekwa sokoni, simu bandia hazifanyiwi majarbio ya ubora na kuna taarifa za kitafiti zinazoonyesha kuwa baadhi ya simu bandia zina kiwango kikubwa cha madini ya risasi na vitu vingine ambavyo ni hatari kwa mazingira na afya ya binadamu. 

Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa simu feki zinatengenezwa na
malighafi dhaifu zisizokidhi viwango na zimeshaonesha kuwa kiwango cha hatari cha vyuma na kemikali kama risasi hadi kufikia kiwango cha mara 40 zaidi kuliko kiwango kilichoidhinishwa na sekta ya mawasiliano duniani kwa mujibu wa na Jukwaa la Watengenezaji wa Simu za Mkononi (MMF).

Akizungumza kuhusu hatua ya Tigo kutoa tahadhari kwa wateja wake Zakaria alisema, ``Wanunuzi wanatakiwa kuwa waangalifu wakati wanaponunua simu mpya au vifaa vya mawasiliano madukani au katika intaneti kwa sababu bidhaa nyingi feki zinatengenezwa kwa kuigaa muundo na nembo za kibiashara za bidhaa halisi kwa makusudi ili kuwalaghai wateja. 

``Ili kuweza kuelewa iwapo simu yako ni feki au ni halisi unatakiwa kupiga namba namba *#06# ambapo atapokea namba ya IMEI ya simu hiyo na kisha kutima kwa njia ya jumbe mfupi kwenda namba 15090 ambapo utapata jibu iwapo simu hiyo ya mkononi ni halisi au ni bandia,” alisema Zacharia. 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...