Thursday, 18 February 2016

WAZABUNI MBEYA WAIDAI SERIKALI BILIONI1.3

Na Esther Macha, Mbeya

WAZABUNI wa wanaotoa huduma za chakula katika taasisi za serikali Mkoani Mbeya wamemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli awasaidie kulipwa fedha zao ambazo wanaidai serikali zaidi ya Bil.1.3

Wamesema kuwa fedha hizo ambazo ni madeni yanayotokana na kutoa huduma ya chakula katika vyuo vya afya Mikoa ya Mbeya ,Rukwa pamoja na magereza hivyo kitendo cha serikali kuchelewa kuwalipa fedha zao tangu mwaka 2009 kumesababisha wazabuni wengine kufilisika na kuuzwa nyumba zao .

Kauli hiyo imetolewa jana Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wazabuni Mkoa wa mbeya ,Yahaya Lema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na madeni hayo .

Lema alisema kuwa anashangazwa na serikali kutoona umuhimu wa kulipa madeni hayo wakati tayari yalishahakikiwa hivyo kutokana na hali hiyo wamemuomba Rais Magufuli awasaidie ili waweze kupata fedha zao.

“Tuna imani na Rais Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia watu hivyo hata hili tunajua atasikia kilio chetu cha muda mrefu ,nina hakika tutalipwa fedha zetu”alisema Lema.

Aidha Lema alisema kuwa licha ya serikali kuchelewesha kulipa fedha zao wazabuni bado wameendelea kutoa huduma ya chakula taasisi ambazo wanazidai .

Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa wazabuni hao,Frank Mwakang’ata alizitaja taasisi sugu ambazo wanazidai kuwa ni Chuo cha afya Mbeya,Chuo cha Tukuyu,Afya Mbozi,AfyA (CATC) Sumbawanga,chuo cha ufundi magereza pamoja na magereza yote ya Mkoa wa Mbeya.



Akizungumzia madeni hayo,Katibu wa chuo cha afya Mbeya,Mkola Juma alisema hana taarifa zozote za deni hilo na kwamba amefika wakati mfumo wa huduma ya chakula umebadilishwa .

Kwa upande Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani hapa SACP,Julius Sang’udi alisema ni kweli taasisi hiyo inadaiwa na madeni hayo yameshapelekwa makao makuu kwa ajili ya kuhakikiwa 


******************************************************


Na Esther Macha, Tunduma

HALMASHAURI ya mji wa tunduma imefanikiwa kuongeza mapato katika chanzo cha usafi wa mazingira cha custom kutoka shilingi milioni 37 mpaka kati ya shilingi milioni 70 na 75 kwa mwezi.

Ongezeko hilo limepatikana katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2015/ 2016 baada ya halmashauri kumtoa mzabuni aliyekuwa akikusanya mapato katikla chanzo hicho na kuisimamia yenyewe kazi hiyo.

Akizungumza na majira ,Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Tunduma , Halima Mpita alisema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 halmashauri ililenga kukusanya shilingi milioni 769 kutoka katika chanzo hicho na ilipo malizika nus u ya kwanza ta mwaka huo wa fedha imefanikiwa kukusanya shilingi ,milioni 354

Alisema makusanyo hayo ni asilimia 84.6 ya lengo na kwamba huenda halmashauri ingefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia mia moja ama zaidi lakini changamoto cha kiutendaji pamoja na sheria za usafirishaji wa mizigo inayovushwa katika mpaka huo nyakati za usiku zimechangia kukusanywa kwa kiwango hicho.

Mpita alikuwa akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma, ally mwafongo juu ya ubadhirifu unaofanywa na watumishi wa halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato wa chanzo hicho .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tunduma , mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,Ally Mwafongo alisema fedha inayokusanywa haina uhalisia na taarifa ya makusanyo hayo inayo wasilishwa kwenye vikao vya baraza la madiwani.

Alisema uchunguzi alioufanya kupitia taarifa ya idadi ya magari yanayopita mpakani hapo iliyo thibitioshwa na mamlaka ya mapato , tra, katika mpaka huo katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2015/2016 kuna upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 171.8

Hata hivyo mpita alisema anatanbua madiwani hawana imani na wataalamu wa halmashauri hivyo kuanzia mwishoni mwa mwezi huu halmashauri itaanza kukusanya mapato yake kwa njia ya mtandao



Mwisho.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...