Mbuyi Twite akitolewa nje baada ya kuumia |
Mashabiki wa Yanga Sc wakishangilia ngoli ya Vincent Bossou |
Golikipa wa Mbeya City Juma Kaseja akipapangua goli, |
Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari cha Yanga na Msemaji wa klabu hiyo, Yanga Jerry Muro (kulia) akiwa na Meneja wa Simbayablog Friday Simbaya.
|
Amissi Tambwe amefunga boa lake la 21 leo, akimfunga kipa mkongwe nchini Juma Kaseja.
Tambwe raia wa Burundi amefunga bao hilo likiwa ni la pili kwa Yanga katika mechi ambayo wameshinda kwa mabai 2-0 dhidi ya Mbeya City.
Bao lake hilo la 21 msimu huu ni gumzo, sasa anamuacha mshambuliaji Mganda wa Simba, Amissi Kiiza kwa mabao mawili kwa kuwa ana 19.
Tambwe amefunga bao hilo akiwa umbali wa takribani mita 23, ilikuwa kama anatuliza lakini tayari alijua Kaseja alikuwa amesogea mbele, akaachia shuti lililojaa wavuni moja kwa moja.
GOOOOOOO Dk 15, Bossou anaunganisha mpira wa kichwa wa krosi ya Abdul na kuandika bao kwa Yanga. Kwa udhamini wa Maji Africa
MBEYA: YANGA imezidi kuupendezesha ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya jana Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga sasa inafikisha pointi 71, baada ya kucheza mechi 28 na ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Ndanda FC na Majimaji kukamilisha msimu.
Hadi mapumziko, tayari Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na beki Mtogo, Vincent Bossou.
Bossou alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 15, akimalizia krosi ya beki mwenzake, Juma Abdul kutoka kulia aliyeanzishiwa kona fupi na winga Simon Msuva.
Amissi Tambwe akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili
Hata hivyo, Yanga ilipoteza wachezaji wake wawili kipindi cha kwanza, mfungaji wa bao Bossou na kiungo Mkongo Mbuyu Twite ambao wote waliumia.
Nafasi ya Twite ilichukuliwa na Salum Telela dakika ya nane na Kevin Yondan alichukua nafasi ya Bossou dakika ya 29.
Kwa ujumla Yanga ilitawala mchezo kipindi cha kwanza na ingeweza kuondoka inaongoza kwa mabao zaidi kama si kosakosa za wazi mbili tatu.
Kipindi cha pili, nyota ya wana Jangwani iliendelea kung’ara na kuzidi kuwafunika wenyeji Mbeya City uwanjani.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe akafunga bao lake la 21 katika Ligi Kuu msimu huu kuipatia Yanga bao la pili dakika ya 85 kwa shuti la nje kla 18.
Mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma hakuwa mwenye bahati kutokana na kukosa mabao mawili ya wazi, moja kila kipindi wakati Simon Msuva alipoteza nafasi moja nzuri kipindi cha pili.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya.
Mbeya City; Juma Kaseja, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Tumba Swedi, Haruna Shamte, Kenny Ally, Suleiman Mangoma/Hamidu Mohamed dk66, Ramadhani Chombo ‘Redondo/Raphael Alpha dk46, Salvatory Nkulula, Geoffrey Mlawa na Joseph Mahundi/Ditram Nchimbi.
No comments:
Post a Comment