Monday, 4 July 2016

TECNO WAZINDUA SIMU KALI YA CAMON C9


MENEJA MAUZO KUTOKA KAMPUNI YA TECNO MOBILE FRED KADELANE AKIONYESHA SIMU HIYO MARA TU BAADA YA KUZINDUA. WATEJA MIA MOJA WA KWANZA WALIFANIKIWA KUPATA SIMU ZAO.
Tecno Mobile imezindua simu mpya aina ya CAMON C9 yenye uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa


Tecno Camon C9 iliyoanza kuuzwa toka tarehe 25 Juni 2016. Ina uwezo wa hali ya juu katika suala zima la kupiga self na kwamba ni simu ya kijanja inayoendana na kasi ya mabadiliko ya Teknlojia ya simu.


Akizindua simu hiyo meneja mauzo toka Tekno Fredy Kadelane amesema simu hiyo imekuja kukidhi haja ya wateja wanaotaka vitu vyenye viwango vya juu, akisistiza simu hiyo kuwa ni Zaidi ya simu.


“Kama mpenzi wa picha Camon C9 imekupa Camera unayoihitaji kwani inaweza kutambua sura na kupiga selfie kali hata ukiwa gizani. Pia Camera yake ina urembo wa kweli (make-up) ambayo itafanya picha zako kuwa na mvuto wa asili.” Alisema Kadelane

Ameongeza kusema Tecno Camon C9 ina uwezo wa kujaza watu wengi kwenye selfie moja jambo ambalo ni tofauti na simu yoyote ile duniani. Camera ya C9 inachukua angle kubwa zaidi hivyo kukuwezesha kupata selfie nzuri ya watu wengi zaidi. 


Ametaja sifa nyingine ya Simu ya Camon C9 kuwa ina Iris recognition Inayosaidia mmiliki wa simu kuweza kufunga simu yake na kufungua kwa njia ya kuitazama badala ya kuweka neno la siri (Password) kama ilivyozoeleka katika simu zingine.


“Sasa hakutokuwa na sababu ya kuweka password, Tecno inatumia teknolojia mpya ya IRIS recognition ambayo inatumia macho kufungua simu. “ alisema


WATEJA 100 WA KWANZA WAPEWA SIMU ZAO


Aidha wateja 100 wa kwanza ambao walifanya zoezi la ku order mapema simu hizo wamefanikiwa kupewa simu zao katika showroom ya Tecno iliyopo duka la City Mall jijini Daresalaam.


“Uzinduzi huu unaenda sambamba na kutoa simu kwa wateja wetu miamoja wa kwanza waliyofanya manunuzi ya awali (pre-order) katika show room zetu zilizopo City Mall, Clock tower na Mobile plaza ghorofa ya pili.”Alisema 


Aidha akifafanua jinsi wateja wa awali walivyoshiriki kufanya manunuzi ya awali, Amesema wateja hao walifanya malipo ya awali ya Tsh. 30,000 na kupewa kadi ya “huduma kwa wateja kutoka” Tecno na kifurushi cha zawadi (gift hamper) za bidhaa kutoka Tecno. 


Kadi ya huduma kwa wateja itatumika katika kutengenezewa simu katika duka zetu za Tecno baada ya kujipatia simu yenyewe. 


WATEJA WAIPA KONGOLE TECNO MOBILE


Kwa upande wao wateja waliofika katika duka la city mall kuchukua simu zao hawakusita kuonyesha furaha yao baada ya kupokea simu hizo wakisema simu hizo zinaendana na wakati wa sasa na kwamba gharama yake ni nafuu ukilinganisha na ubora wa simu yenyewe.


Akizungumza na Fullhabari.com, mmoja wa wateja hao Bw.Harrison Ndungulile amekili kwa kusema simu hiyo ya common c9 imekuja kukidhi haja za watu wanaopenda zimu za smartfone

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...