Wednesday, 23 November 2016

ASILIMIA 90 YA VIJIJI VYA WILAYA YA MUFINDI HAVINA ARDHI YA AKIBA


Wanafunzi wa shule ya msingi Kilimahewa katika Kijiji cha Usokami katika Kata ya Kibengu wilayani mufindi mkoani iringa akipita jirani na mkutano mkuu wa kijiji wakiwa wamejitwisha ndoo za maji baada ya kutoka shuleni jana. Kijiji cha Usokami kinakabiliwa na tatizo la maji safi na salama kutokana na kijiji hicho kutokuwa kuwa na mradi wowote wa maji ya bomba. (Picha na Friday Simbaya)






Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mufindi, Simon Mbago

MUFINDI: Asilimia 90 ya vijiji vya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa havina ardhi ya akiba kwa ajili ya uwekezaji na shughuli mbalimbali za kiserikali, Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mufindi, Simon Mbago ameelezea.

Alisema kuwa migogoro mingi ya ardhi inayotokea kwenye vijiji wilayani humo ni kukosekana kwa ardhi ya akiba kwa ajili shughuli za maendeleo na uwekezekaji.

Akiwasilisha mada katika mdahalo uliofanyika jana katika Kijiji cha Usokami, Kata ya Kibengu wilayani humo alisema kuwa migogoro hiyo itakoma endapo vijijji husika vitatenga ardhi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Huu ni mdahalo wa saba tangu kuanza kutolewa kwa midahalo hiyo inayoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la TAGRODE lenye makao yake mkoani Iringa inayolenga kutafuta mambo yakufanya ili kupunguza migogoro ya ardhi katika wilaya za Iringa na Mufindi mkoani Iringa.

Shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la PELUM Tanzania la mkoani Morogoro, linaendesha midahalo hiyo katika vijiji vya Ikuka, Mbigili, Mawala, Mawambala na Masalali kwa Wilaya ya kilolo.

Na katika vijiji vya Usokami, Ugesa, Makungu, Magunguli na Isaula Wilaya ya Mufindi kupitia mradi wake wa CEGO unaohusisha jamii ya vijijini katika uwajibikaji wa masuala ya ardhi ya kijiji.

Afisa ardhi huyo aliendelea kusema kuwa vijiji kwa kutotenga ardhi ya akiba kunapelekea vijiji hivyo kukosa miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa hospitali, shule na wakezaji.

“Kwa asilimia kubwa ya vijiji vya Wilaya Mufindi havina ardhi ya akiba kunakopelekeaa miradi mingi kuchukua ardhi ya watu binafsi na kusababisha migogoro ya ardhi…,” alisema Mbago.

Afisa ardhi huyo wa Wilaya ya Mufindi wamevishauri vijiji hivyo kutenga ardhi ya akiba ya vijiji ili serikali inapotaka kufanya shughuli yoyote ya kimaendeleo katika kijiji husika miradi huyo ifanywe katika ardhi ya akiba.

Aliendelea kusema kuwa mradi wowote ule hauwezi kuwekezwa sehemu yenye migogoro ya ardhi au kijiji kutokuwa na ardhi ya akiba itapelekwa mahala pengine au kijiji kingine penye ardhi ya akiba.

Wakichangia mada katika mdahalo huo, wananchi wa kijiji cha usokami kata ya kibengu walisema kuwa ili kupunguza migogoro ya ardhi serikali hainabudi kuhakiki mipaka upya ya vijiji na vijiji na wilaya na wilaya.

Pia wananchi hao walisema kuwa serikali za vijiji ni chanzo cha migogoro kwa sababu zina baadhi ya viongozi wanaoshindwa kusimamia sheria hizo baada ya maamuzi kufanywa.

Wananchi hao wa kijiji cha usokami waliomba serikali kuhakiki mipaka ya kijiji chao pamoja kupelekewa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Usokami Franciso Kaguo aliomba serikali kwa kutumia sheria hizo kutenga maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji hatua itakayosaidia kuepukana na migogoro kwa kuwa makundi yote mawili yanategemeana.

Wakati huohuo, Kijiji cha Usokami wilayani Mufindi, mkoani Iringa kunakabiliwa na tatizo la maji safi na salama kutokana na kijiji hicho kutokuwa na mradi wowote wa maji.

Wananchi hao wa kijiji hicho wanatumia maji ya visima na kuiomba serikali iwapelekee mradi wa maji ya bomba ili kunusuru afya za wakazi hao.

Walisema kuwa miradi yote ya maji haifanyi kazi na kulazimika kutumia muda mwingi kutafuata maji katika visima vya watu binfasi.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...