Muuguzi Mwandamizi wa Zahanati ya Ugesa Theresia Augustino Chaula |
MUFINDI: Muuguzi Mwandamizi wa Zahanati ya Ugesa katika Kata ya Ihalimba wilayani Mufindi, mkoani Iringa Theresia Augustino Chaula wanawake wengi wanatoa mimba kiholela hali inayopelekea vifo kwa mabinti na wanawake waliopo kwenye ndoa.
Alisema kuwa tatizo la utoaji mimba katika kijiji cha Ugesa ni kubwa na wanakuja hospitali wakiwa na hali mbaya kiafya baada ya kutoa mimba mitaani.
“Wanawake wengi wanaofika hospitalini hapo wanadai mimba imetoka yenyewe wanaogopa kukosa huduma…,” alisema Chaula.
Chaula alisema jana wakati akiongea na Nipashe kuwa kuna baadhi ya wanawake hujaribu kutoa mimba kwa kuingiza vifaa vyenye ncha kali au vitu vichafu tumboni au kwa kujipiga makonde tumboni.
Alisema kuwa mojawapo ya madhara makubwa ambayo yanampata mwanamke anayetoa mimba vichochoroni ni kutokwa na damu nyingi na kupasuka kwa kizazi.
Alisema kuwa vitendo hivi ni hatarishi na kamwe mwanamke yeyote asifanye hivyo, kwa kuwa vinaweza kusababisha majeraha yenye athari kubwa tumboni, ikiwa pamoja na kuvuja damu nyingi na hivyo kuleta kifo.
Alisema wapo wanawake wanaotoa wasichana na wanawake mimba kwa kuingiza vifaa vyenye ncha kali au vitu vichafu tumboni.
Alisema kuwa Kijiji cha Ugesa kina tatizo la ngono zemba kutokana na ulevi wa pombe za kinyeji aina ya Ulanzi.
“Katika msimu huu wa pombe watu wamekuwa wakishiriki ngono zembe kunakopelekea mimba zisizotarajiwa na hatimaye kutoa mimba kiholela…,” alisema Chaula.
Alisema kuwa anakusudia kuitisha mkutano wa kijiji ili kuwabaini watu wanaotoa (maarufu kama ngariba) mimba mabinti na wanawake ili wachukuliwe hatua.
Wakati huohuo, muuguzi mwandamizi huyo, alisema zahanati hiyo inaupungufu wa watumishi wa afya ambapo aliongeza kuwa kwa pekee yake hataweza kulingana wingi wa wagonjwa wanaofika kwa matibabu.
Alisema kuwa ili huduma za afya ziendelee kwa ufanisi kunahitaji kuwepo na muuguzi mmoja, tabibu msaidizi mmoja na mhuduma mmoja.
Kijiji cha Ugesa ni moja ya vijiji ambavyo kwenye mradi wa kuendesha midhalo kuhusu migogoro ya ardhi inayotekelezwa na Shirika la TAGRODE kwa kushirikiana na shirika la PELUM Tanzania la mkoani Morogoro.
Shirika hilo linaendesha midahalo hiyo katika vijiji vya Ikuka, Mbigili, Mawala, Mawambala na Masalali kwa Wilaya ya kilolo.
Na katika vijiji vya Usokami, Ugesa, Makungu, Magunguli na Isaula Wilaya ya Mufindi kupitia mradi wake wa CEGO unaohusisha jamii ya vijijini katika uwajibikaji wa masuala ya ardhi ya kijiji.
No comments:
Post a Comment