Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa matamasha ya Mtikisiko yanayolenga kunyanyua sekta ya muziki yatakayofanyika katika mikoa katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya kwa uratibu wa radio ya Ebony FM
Iringa: Kampuni inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imesaini rasmi uzinduzi wa tamasha la mwaka la Mtikisiko kwa kushirikiana na kituo cha redio cha Ebony FM ambacho kina wasikilizaji wengi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Mtiririko wa matamasha hayo ya mwaka unatarajiwa kuanza Novemba 19 hadi 26 katika mikoa ya Njombe na Mbeya kwa pamoja ambapo onesho la fainali litafanyika Desemba 10, 2016 mkoani Iringa.
Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkoani Iringa, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga alisema, “Tigo kila mara inakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba vipaji vinavyoibukia katika sekta ya muziki vinapewa jukwaa la kuonesha vipaji vyao na wasanii maarufu wanaweza kuunganishwa na mashabiki wao.
Tamasha la Mtikisiko linakuja baada ya kumalizika kwa Tamasha la Tigo Fiesta 2016 hivi karibuni ambalo Tigo ilikuwa mdhamini mkuu. Kiswaga aliwaaambia waandishi wa habari kwamba mashabiki watarajie ubora ule ule wa burudani waliouzoea wakati wa tamasha la Fiesta.
Kushiriki kwa Tigo kutakwenda sambamba na kuhakikisha wateja wa Tigo na wale ambao sio wateja wanafahamu na kuzielewa huduma za Tigo wakati wa tamasha.
“Katika kukuza uzoefu wa mteja na mtumiaji wakati wa tamasha, tunatarajia wateja wetu kutumia vilivyo kuanzishwa kwa huduma ya 4G LTE, Tiogo Pesa na bidhaa na huduma nyingine zinazotolewa,” alisema Kiswaga.
Kiswaga alitangaza kuwa washiriki wa tamasha hilo kwa mwaka huu watakuwa na nafasi ya kuchagua njia ya kupata tiketi zao kupitia Tigo Pesa bila gharama ya ziada.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo washiriki wote wa tamasha ambao watanunua tiketi zao kupitia Tigo Pesa watafurahia faida kwa kupata [punguzo la asilimia kumi kwa kila tiketi itakayonunuliwa
Kiswaga alifafanua, “Kununua tiketi kupitia Tigo Pesa, wateja kutoka mtandao wowote watapiga namba ya Mfumo wa Kifedha wa Simu (mfano *150*01# kwa Tigo), halafu chagua, “tuma pesa”, ikifuatiwa na chagua, “Mitandao Mingine” halafu chagua, “Tigo Pesa” na mwisho ingiza namba 0674444444.
Kwa upande wake mratibu wa Tamasha la Mtikisiko 2016, Austine Nyondo alisema, “Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaashukuru Tigo wakiwa ni wadhamini wakuu wa tamasha hili; mashabiki wetuwatarajie kupata burudani kutoka kwa wasanii maarufu katika sekta ya muziki.”
Aliarifu kuwa wakati wa tukio hilo watasambaza vipeperushi kwa vijana ambavyo vitakuwa na ujumbe unaohusu Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutokana na sababu kwamba mikoa ya kusini inachukuliwa kuwa ni “ukanda ulioathiriwa” na janga hilo.
Tamasha maarufu la Mtikisiko ambalo awali lilijulikana “Together Time” lilibadilishwa jina mwaka 2008 lilianza mwaka 2007 na limeendelea kukua katika kipindi chote cha miaka hiyo na kupata umaarufu kama tamasha la burudani la mwisho wa mwaka katika mikoa ya kusini.
No comments:
Post a Comment