Wednesday, 21 December 2016

JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LAJIPANGA KUKARIBILIANA NA VITENDO VYA UHALIFU

Image result for RPC IRINGA JULIUS MJENGIImage result for RPC IRINGA JULIUS MJENGI

Jeshi la Polisi mkoani Iringa lasema limejipanga kukabiliana vitendo vyote vya uhalifu kuelekea katika kipindi cha sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya na kuonya kuwa kamwe watu wasidhubutu kufanya fujo.

Akiongea na SIMBAYABLOG leo  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamshina Msaidizi wa Polisi (ACP), Julius Mjengi alisema kuwa jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na vitendo vyote vya kihalifu.

Alisema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara na nyumba za ibada.

Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kikristo hutumia muda huo kwenda kuabudu siku ambayo wanakumbuka kuzaliwa Yesu Kristo pamoja na mwendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. 

Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. 

Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani, alisema kamanda huyo.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi litamarisha doria maeneo yote hapa mkoani pamoja na kufuatilia mienendo na kukamata watu wote wataochochea, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo.

“Tukiwa katika kipindi hiki cha kusherehekea Krismasi na Mwaka Mpya, nawaomba wananchi mkoani hapa kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha ulinzi na usalama mkoani hapa vinaimarishwa na wale wote watakayebainika kufanya uhalifu wanakamatwa na sheria ichukua mkondo wake,” alisema kamanda Mjengi.

Alisema kuwa jeshi la polisi pia itaimarasha usalama katika nyumba zote za ibada na kuwaomba waumini kutoa ushirikiana kwa jeshi hilo.

Katika hatua nyingine, jeshi la polisi limepiga marufuku vitendo vya kuchoma matairi, kukimbizi magari huku madereva wakiwa wamelewa pamoja na kupiga mafataki.

Jeshi hilo limesema kuwa litahakikisha watu wanasherehekea siku hizo mbili za krismasi na mwaka mpya kwa amani na utulivu.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...