Timu ya Soka ya Kiponzelo ya Kijiji cha Kiponzelo, Kata ya Maboga, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa imeibuka mshindi dhidi ya wapinzani wake Timu ya Soka ya Makongati ya Kijiji hicho kwa kuilaza magoli 3-0 kwenye pambano la ufunguzi ya Kombe la J.Msofu lililopigwa katika Uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Kiponzelo jana.
Mashindano ya Kombe hilo lililoandaliwa na Jeremia Edward Msofu ambaye pia ni mmliki wa kampuni ya mabasi ya ‘OTA HIGH CLASS’ kwa kushirikiana na chama cha mpira wilayani Iringa lilioanza rasmi tarehe 11 Desemba 2016.
Timu ya Soka ya Kiponzelo wenyeji waliovalia jezi ya rangi nyeusi walijipatia goli la kwanza kupitia mshambuliaji wao machachali Efeso Makaye (9) ambaye ndiye alikuwa nahodha wa timu hiyo dakika 44 katika kipindi cha kwanza.
Hadi mapumziko timu ya kiponzelo ilikuwa inaongoza kwa goli moja lakini kipindi cha pili kilipoanza timu zote zilishambuliana na kupelekea timu ya kiponzelo kupata goli la pili kupitia mshambuliaji wake aliyefunga bao la kwanza dakika chache kwa kuanza kipindi cha pili.
Wakati timu ya soka ya Makongati ya kijiji cha Makongati waliovalia jezi ya rangi ya zambarau, Kata ya Maboga haijakaa sawa waliongezwa goli la tatu wakati huo kupitia uwinga wa kulia wa timu ya kiponzelo Yesus Mamba.
Mechi ya ufunguzi hiyo ya Kombe la J. Msofu ilichezeshwa na mwamuzi Ahmad Mzee akisaidiana na wasaisizi wake steven Makuka na Daud Mgimba.
Kwa upande wake, mdhamini wa mashindano hayo Jeremia Msofu alisema kuwa lengo la mashidano hayo nikuibua vipaji vitakavyoweza kuunda timu ya Jimbo la Kalenga itakayoweza kucheza kuanzia ligi ya daraja la nne la hadi ligi kuu Tanzania (VPL).
Alisema kuwa mashindano hayo hayana mlengo wa kisiasa, bali ni kuibua vipaji na isitoshe yeye ni mzaliwa wa Kijiji cha Kiponzelo Kata ya Maboga katika Jimbo la Kalenga wilayani Iringa,mkoani Iringa.
“Kwa kuanzia nimeamua kuanza na kata mbili ambazo zinajumlisha vijiji vinane lakini hapo baadaye nakusudia kufanya kwa Jimbo la Kalenga lote Mungu akipenda…” alifafanua Msofu.
Msofu alitoa vifaa vya michezo kwa kila timu shiriki kwa kupewa jezi seti moja na mpira moja kwa kila kijiji kushiriki.
Naye mratibu wa mashindano hayo Abuu Changawa ‘Majeki’, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Lipuli FC ya mjini Iringa aliwasisitizia wachezaji wanaoshiriki Kombe la Jeremia (J.MSOFU CUP 2016) kuzingatia nidhamu.
Aidha, mratibu huyo alisema kuwa jumla ya vijiji nane kutoka kata ya maboga na Wasa, ambavyo ni Wasa, Usengelindete, Ufyambe na Ikungwe, (kata ya Wasa), Kiponzelo, makongati, Magunga na Itengulinyi vya kata ya Kiponzelo vinashiriki katika kombe hilo.
Kwa upande wa zawadi mratibu huyo alisema kuwa mshindi wa kwanza atapa ng’ombe mmoja, mshindi wa pili mbuzi wawili na mshindi wa tatu atapata mbuzi mmoja na kuongeza kuwa gharama ya mashindano hayo ni zaidi ya shilingi milioni kumi.
Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi na Katibu wa Chama cha Mpira Iringa Vijijini ,Juma Lalika, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha Mpira Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment