Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akihojiwa na waandishi wa habari
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa wamezisimamisha Daladala kwa kosa la kupakia abira eneo ambalo sio rasmi
Jinsi magari yanavyogeuza katika eneo la Buhongwa
Eneo la stendi isiyokuwa rasmi ya Buhongwa ilivyo katika kadhia ya ubovu
Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akikagua eneo la barabara ya Buhongwa ambayo inatumiwa na madereva Daladala kama stendi
Gari likigeuza katikati ya barabara kutokana na kukosekana kwa eneo maalumu la stendi
Wajasiriamali wakiwa katika eneo la biashara huku Daladala zikitumia eneo hilo pia kupakia na kushusha abiria
Gari inageuza kituoni ambapo ni barabarani huku watu wakiendelea kuvuka barabara
Dede akikagua barabara iliyoharibika
Gari ikiwa imepaki katika eneo bovu la barabara ya Buhongwa
Mwandishi wa habari wa www.wazo-huru.blogspot.com Mathias Canal akimhoji moja ya madereva katika eneo la Buhongwa
Mwenyekiti wa madereva Kanda ya ziwa Bw Hassan Dede akisalimia na wakazi wa eneo la Nyashishi mara baada ya kuzuru katika eneo hilo ambalo ndilo amependekeza kuwa stendi ya daladala, kushoto kwake ni Mwandishi wa habari wa www.blogspot.com Ndg Mathias Canal
Na Mathias Canal, Mwanza
Uongozi wa Mkoa wa Mwanza umetakiwa kubainisha stendi za Daladala, maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara za mbogamboga na matunda kwa kina mama sambamba na kubainisha maeneo maalumu ambayo daladala haziruhusiwi kusimama kwani kufanya hivyo kutaondoa urasimu uliopo baina ya madereva wa Daladala na askari wa usalama barabarani.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa madereva Kanda ya ziwa Bw Hassan Dede wakati alipozuru kujionea kadhia wanazokumbana nazo madereva wawapo barabarani sambamba na kujionea kandia wanayoipata kutokana na ubovu wa barabara na kutokuwa na stendi ya Daladala katika Mtaa wa Buhongwa nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana.
Dede alisema kuwa ni ajabu kwa nchi yetu kuwa na kituo cha daladala chenye mwanzo lakini hakina mwisho hivyo kuwafanya madereva kugeuza mahala pasipokuwa rasmi ambapo ni hatari kwa uhai na magari na madereva hao.
Katika eneo la Buhongwa zinapogeuzia daladala kama kituo, barabara yake ni mbovu huku pembeni kukiwa na machinga sambamba na wajasiriamali wanaouza mbogamboga na matunda jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa wafanyabiashara hao endapo kama g
No comments:
Post a Comment