Monday, 9 January 2017

VIJANA NCHINI WAASWA KUJITUMA NA SIO KUKAA BURE…






Bwana John Massao na Theresia Massao wakiwa katika mmoja ya mizinga walioweka katika msitu wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa eneo la Gangilonga, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)





IRINGA: VIJANA nchini wanatakiwa kujishughulisha na ufugaji wa nyuki kisha kujikwamua kimaisha kwa kuongeza kipato, kiuchumi kuliko kutegemea serikali kuwatafutia ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa TEJO’s Honey, John Massao jana wakati akiongea na nipashe, ambao niwazalishaji na wasindikaji wa asali asilia mjini iringa. 

Massao alisema kuwa vijana ndio kundi kubwa lisilokuwa na ajira wala mapato katika mfumo wa maisha na wanahitaji kujiajiri kwa kutumia rasilimali na maliasili zilizoko katika mazingira yao.

Aliwataka vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya pamoja na kuanzisha ufugaji wa nyuki na kuweza kupata asali na nta kisha kupata soko litakalosaidia kujiinua kiuchumi na kuongeza mapato katika familia ikiwa ni pamoja na kuepukana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kuvunja sheria. 

Alisema kuwa vijana wasisubiri ajira za maofisini tu kumbe wange tumia rasilimali ya misitu kufuga nyuki kuliko kubaki maisha tegemezi na ombaomba kumbe wangeweza kutumia ardhi na misitu ya asili jirani na hifadhi za Taifa.

“Nchi hii ina mapori mengi lakini vijana wakijiunga kwa pamoja kwa kuweka mizinga katika mapori ambayo utasaidia kuhifadhi misitu na mioto,” alisema Massao.

Alisema kuwa asali ikivunwa inadumu kwa muda mrefu mpaka miaka 100 na haiitaji kupaliliwa wa kuweka mbolea kama shambani, kwa hiyo vijana watumia fursa waingie katika soko la ufugaji.

Awali Mkurugenzi wa TEJO’s Honey, Theresia Massao aliitaka serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha jamii kufuga nyuki kwa kutumia njia za kisasa na kuzalisha kwa wingi zao hilo .

Theresia alisema takwimu inaonesha Tanzania ina misitu mingi ambazo ni makazi ya makundi ya nyuki na ikitumika vizuri na vijana kufugia nyuki kwa kuzalisha asali itainua kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

“Kutokana na ufugaji wa nyuki jamii inaweza kujipatia gundi ya nyuki , sumu ya nyuki inayotumika katika tiba pamoja na maziwa ya nyuki kama chakula na tiba “alisema Theresia.

Vilevile alifafanua kuwa wananchi kwa kufuga nyuki wataweza kuboresha afya za familia kwa sababu asali inatumika kama chakula na tiba kwa magonjwa mbalimbali kama vile vidonda vya tumbo na kansa.

Katika hatua nyingine aliwaasa wananchi na wafugaji kujiepusha na uharibifu wa mazingira kwa kuchoma na kukata miti na makazi ya nyuki kwa kukosa maua na maji kisha kuzalisha kiwango kidogo cha asali na nta na hata kuhama katika mizinga baada ya kupata usumbufu wa makazi kimazingira.

TEJO ni muuganiko wa majina mawili yaani, Theresia na John (TEJO) ambao ni mume na mke walieamua kuanzisha kampuni hiyo baada ya kustaafu utumishi wa umma kama maofisa misitu.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...