Thursday, 20 April 2017

MAKOTA FOREST YAKABIDHI BATI 20 NA MIFUKO YA CEMENT 100 KWA MKUU WA WILAYA KILOLO



Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah (kushoto) akipokea msaada wa madawati 20 kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya Makota Forest Bharat Bhesania jana kampuni hiyo imetoa madawati hayo pamoja na bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.





KAMPUNI ya Makota Forest ya inayojihusisha na shughuli za Kilimo katika kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetoa msaada wa bati 100 pamoja na madawati 20 kwa ajili ya kuunga mkono serikali ya wilaya ya Kilolo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa .


Akizungumza leo [jana] wakati wa kukabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ,Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bharat Bhesania alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika wilaya ya Kilolo na maeneo mengine ya mkoa wa Iringa .


Bhesania alisema kuwa jitihada zinazofanywa na viongozi wa wilaya ya Kilolo na mkoa wa Iringa katika kuwaletea wananchi maendeleo ni jitihada ambazo zinapaswa kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo ndani ya mkoa huo na waliopo nje ya mkoa .


" Sisi kama wawekezaji tunaowajibu wa kuunga mkono shughuli zote za kimaendeleo zinazoendelea katika maeneo yetu ....nimekuwa nikisaidia shughuli nyingi sana na sichoki kuendelea kusaidia "Alisema Bhesania


Kwa pande wake Meneja wa kampuni Gibson Mkuvalwa alisema kampuni yake inajihusisha na kilimo cha mahindi na mwaka huu ndipo shamba hili limeanza ila changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kodi kubwa wanayolipa na kuomba serikali kuweza kuliangalia hilo.


Mkuvalwa alisema kupitia kampuni hiyo wameweza kutoa ajira kwa wananchi wanaozunguka kampuni hiyo na wamekuwa wakijitolea kutengeneza barabara na kushiriki kwa nguvu zote kuunga mkono shughuli za kimaendeleo .


Nae Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia alisema kuwa kuwa mwekezaji huyo ameanza kufungua rasmi mlango wa wawekezaji na wadau wa maenbdeleo Kilolo kuanza kuchangia bati na madawati na kuwa amepata kufanya ziara ndani ya wilaya hiyo na nje ya wilaya kwenda kuwaomba wawekezaji na wadau wa maendeleo waliopo nje ya Kilolo kusaidia harambee hiyo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu .


Alisema kuwa msaada huo wa kampuni ya Makota Forest ni mwanzo wa wadau wengine kujitokeza kusaidia harambee hiyo na kuwaomba wawekezaji wengine kujitokeza .


Hezron Nganyagwa ni Diwani wa kata ya Ihimbowilayani humo nae aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo alisema kuwa utasaidia kwa matumizi ya shule iliyokumbwa na maafa ya kuezuliwa ambayo wananchi wameanza ujenzi wa kuta .

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...