Thursday, 20 April 2017

MADEREVA 20 KUSHIRIKI MASINDANO YA MAGARI MKOANI IRINGA


Mshiriki wa mashindano ya mbio za magari kutoka Iringa (Mkwawa Rally Team), Ahmed Huwel ambaye atatumia gari lake mpya aina ya Ford Fiesta akimkaribisha Dereva mkongwe wa mbio za magari nchini Gerald Miller (wa pili kulia) kutoka mkoani Arusha alipowasili jana, kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari yatakayofanyika kuanzia tarehe 22-23, mwezi Aprili mwaka huu mkoani Iringa. Mashindano hayo yanayoandaliwa na klabu ya mbio za magari ya Iringa (IMSC) kwa kushirikiana na kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa. (Picha na Friday Simbaya)


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wanahabari jana kuhusu Mashindano ya mbio za magari kitaifa yatakayoshirikisha madereva 20 wakiwa pamoja na wasaidizi wao kutoka ndani na nje ya nchi yanayoandaliwa na klabu ya mbio za magari ya Iringa (IMSC) kwa kushirikiana na kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa IMSC Hamid Mbatta na kushoto kwake ni Afande Steven Nyandongo wa kikosi cha usalama barabarani -Iringa na Mwasisi wa mashindano hayo mkoani Iringa Francis Mwakatundu.(Picha na Friday Simbaya)

Dereva mkongwe wa mbio za magari nchini Gerald Miller kutoka mkoani Arusha akikagua gari lake aina ya Mitsubishi baada ya kuwasili mjini Iringa jana kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari yatakayofanyika kuanzia tarehe 22-23, mwezi Aprili mwaka huu mkoani Iringa. Mashindano hayo kitaifa yatashirikisha madereva 20 wakiwa pamoja na wasaidizi wao kutoka ndani na nje ya nchi yanayoandaliwa na klabu ya mbio za magari ya Iringa (IMSC) kwa kushirikiana na kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa. (Picha na Friday Simbaya)


Mwenyekiti wa chama cha mbio za magari mkoa wa Iringa (IMSC) Hamid Mbatta amewataka wananchi mkoani iringa kutumia fursa ya mashindano ya mbio za magari kukuza biashara kutokana na wageni wengi watakaofika mkoani hapa kushuhudia mashindano hayo.

Alisema kuwa zaidi ya wageni 500 na madereva 20 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajia kushuhudia na kushiriki mashindano ya mbio za magari kitaifa yatakayofanyika mkoani iringa kuanzia tarehe 22-23, Aprili mwaka huu.

Mbatta alisema kuwa mashindano ya magari ni fursa kubwa kwa kufanya biashara pamoja na kukuza na kuimarisha sekta ya utalii kanda ya kusini.

Alisema kuwa kuna njia tano zilizochaguliwa kwa ajili ya mashindano ambapo zaidi ya Km 302 (completion section na transport section) kuanzia kiwanda cha maji cha mkwawa kilichopo mjini iringa ambao ni wadhamini wakubwa wa mashindano hao.

Alitaja washiriki kutoka mkoani Iringa (Mkwawa Rally Team) kuwa ni ahmed Huwel akiwa na msaidizi wake Maisam Fazal ambaye alitumia gari lake mpya aina ya Ford Fiesta na Hamid Mbatta akiwa na msaidizi wake (navigator) sultan Chana.

Mwingine aliyeomba aliomba kushiriki kupitia Mkwawa Rally Team ni Shanto ambaye atakuwa na msaidizi wake Rahim.

Mwenyekiti wa chama cha mbio za magari mkoa wa Iringa Hamid Mbatta alisema kuwa mkoa wa Iringa hadi sasa umeendelea kufanya vema kwenye mashindano hayo na upo uwezekano mkubwa wa kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mwasisi wa mashindano hayo Francis Mwakatundu alisema kuwa Iringa ni tishio kwa mashindano hayo.

Pia dereva mkongwe wa mbio za magari nchini Gerald Miller kutoka mkoani Arusha na davis Mosha wamethibitisha kushiriki mashandano hayo.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza Amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuchukua tahadhari wakati wa mashindano ya mbio za magari.

Akizungumza jana na wanahabari Kasesela alisema kwa siku ya Jumamosi na jumapili wakati mashindano hayo ya mbio za magari zilizodhaminiwa na kiwanda cha maji Mkwawa kuwa ni sehemu ya ukuaji wa uchumi wa mkoa.

Alisema kuwa kupitia mashindano hayo upo uwezekano mkubwa wa mkoa wa Iringa kuingia katika mashindano ya kimataifa ya mbio za magari.

Pia alisema kupitia mashindano hayo upo uwezekano mkubwa wa kutangaza hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Aidha alisema kuwa kwa wazazi wanapaswa kuwa makini na watoto pamoja na waendesha bodaboda kuacha kufukuza magari ya mashindano.

Naye Afande Steven Nyandongo wa kikosi cha usalama barabarani -Iringa amekitaka chama cha mbio za magari mkoa wa Iringa pamoja na washiriki wa mashindano hayo kuhakikisha wanaweka usalama kwanza ikiwa pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani. 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...