Saturday, 20 May 2017

SBL YAZINDUA BIA MPYA IITWAYO SERENGETI PREMIUM LITE




Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi (kulia) ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bia mpya aina ya Lite akitosti glasi na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kushoto) na mjumbe wa bodi ya SBL, Chris Gachuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.



Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ceaser Mloka,akizungumza katika uzinduzi huo.



Crew nzima ya Kampuni ya PR ya Concept ikiwa katika uzinduzi huo.



Maofisa kutoka SBL wakijadiliana jambo.



Wakati wa utambulisho. Kushoto ni mbunifu wa bia hiyo.



Wasanii wakitoa burudani katika uzinduzi huo.





Mjumbe wa Bodi Chris Gachuma akizungumza katika uzinduzi huo.



Wadau wakiwa kwenye uzinduz huo.



Ni furaha tupu katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza.



Muonekano ya bia hiyo katika chupa.



Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha (wa pili kushoto), akitosti glasi na wanahabari katika uzinduzi huo.





Na Dotto Mwaibale


KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), mojawapo ya kampuni kubwa zinazozalisha bia hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa miaka 20 iliyopita. 


“Bia ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia utaalamu wakisasa. 


Ina ladha kamili inayoburudisha zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa huuzwa rejareja sokoni”, alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuia ya wanywaji wake ambaokwakipindikirefuwamekuwawakitafuta biahalisiyakitanzania.


“Pamoja na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa bia ya Serengeti Premium Lite, nisemekuwani bia halisi ya kitanzania yenye kiburudisho na ladha nyepesi. 


Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa mudamrefu.


Tunaami ni kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishajibia (bremasters) wakitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapokuwa wakifurahia urithi wetu waaina hii ya bia ”, alisema Mehta.


Aliongeza kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite inaubora uleule wa kimataifa sawa na biamama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya medali 10 za ubora wakitaifa na kimataifa.”


Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe, aliisifia kampuniya SBL kwa kuwa inaongoza kwa ubunifu katika sekta ya uzalishaji wapombe nchini, na vilevile akaahidi kuwa serikali itaendelea kutoa msaada kwa sekta ya biashara hapa nchini.


Dk.Mwakyembe ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi, alisema SBL imekuwa ikishiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania akitaja mafanikio mbalimbali za program zake za kuisaidijamii.


“Programu za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi, watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili ya kuuza mazao yao ambapo SBL hununua mazao yao kama malighafi inayotumika kuzalishiabia”, alisema Makamba.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...