MUFINDI" MKUU wa Mkoa wa Iringa (RC), Amina Masenza ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kwa kutukiwa Hati Safi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2016.
Huu ni mwaka wa tano mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya CAG.
Alisema hayo wiki iliyopita kuwa matokeo hayo ni ishara ya kazi nzuri iliyofanywa na madiwani kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri.
Masenza alitoa rai kwa halmashauri hiyo kuwa ushirikiano uliopo uendelee kuimarishwa ili rasilimali za halmashauri ziendelee kutumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.
Sambamba na hilo mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa halmashauri hiyo iongeza juhudi katika ukusanyaji na udhibiti wa mapato ya ndani ya halmashauri ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea.
Kwa mujibu wa taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka 2015/16 Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ilishindwa kukusanya kiasi cha shilingi 335,720,860 kutoka kwenye vyanzo vyako vya ndani.
“Hiki ni kiwango kikubwa ambacho kwa kiasi kikubwa kinaathiri uwezo wa halmashauri wa kutoa huduma stahiki kwa wananchini wake,” alisema Masenza.
Alisema kuwa halmashauri hiyo ihakikishe inaweka utaratibu wa kulipa madeni yanayofikia kiasi karibu shilingi bilioni 1.2 ambayo yanatokana na madai ya makandarasi, watoa huduma mbalimbali na watumishi kama ilivyobainishwa kwenye taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali.
Masenza alisema kuwa halmashauri inatakiwa kuhakikisha kuwa inawajengea uwezo wajumbe wa kamati ya ukaguzi na kuimarisha kitengo cha ukaguzi wa ndani ili kwa pamoja waweze kusaidia katika usimamizi wa mfumo wa udhibiti wa ndani kwa kulinda mapato ya halmashauri sambamba na matumizi mzuri ya fedha.
Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (Mkoa wa Iringa)Willy Joseph Undule ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni za fedha za Umma kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.
Taarifa ya CAG ilibainisha kuwa, bado uwezo wa halshauri kujitegemea upo chini hivyo kuendeleza utegemezi mkubwa kwa Serikali Kuu.
Takwimu zinaonesha wuwezo wa Halmashauri ya Mufindi kujitegemea nis sawa na asilimia tisa (9) tu ya matumizi ya kawaida ya shilingi bilioni 35.2 kwa mwaka 2015/2016 ukiliganisha na mapato ya ndani ya shilingi bilioni 3.1 tu.
No comments:
Post a Comment