Saturday, 15 July 2017

HANSPOPPE ATOA MSAADA WA GARI LA ZIMAMOTO KWA JESHI LA ZMT


Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akimemshukuru Zakaria Hanspope kwa moyo wake wa kurudisha fadhila nyumbani na kuwaomba wananchi kushirikiana na jeshi hilo kufanikisha utendaji wake juzi. Anayeshuhudia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye (kulia). (Picha na Friday Simbaya)








IRINGA: Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye ameziomba Halmashauri za Manispaa, na majiji nchini kutoa kipaumbele cha visima vya kuchota maji ya zimamoto wakati wa ujenzi wa barabara kwenye maeneo yao.

Andengenye ameeleza hayo juzi kwenye hafla ya makabidhiano ya gari jipya la zima moto lenye uwezo wa kujaza lita elfu tano ambalo limetolewa na mfadhili kwa lengo la kutatua changamoto ya gari inayoukabili mkoa wa Iringa.

Kauli ya Kamishana Jenerali wa Jeshi la Zimamoto inatokana na ukweli kuwa miji mingi na majiji ina msongamano wa nyumba huku kukiwa na visima vichache vya kukinga maji wakati wa matukio ya moto na kusababisha ucheleweshaji wa huduma hiyo. I

Akitoa taarifa ya mkoa, Kamanda wa Zima Moto Iringa, Kennedy Komba amesema mkoa wake ulikuwa na magari mawili ambapo moja lilipata ajali hivi karibuni likiwa linaelekea kuzima moto na hivyo msaada uliotolewa na Zakaria Hanspope utakuwa mkombozi.

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza amemshukuru mfadhili huyo kwa moyo wake wa kurudisha fadhila nyumbani na kuwaomba wananchi kushirikiana na jeshi hilo kufanikisha utendaji wake.



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...