Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Mazenza akitoa hotuba leo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi cha kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa hesabu (CAG) zilizoishia tarehe 30 Juni, 2016. Kutoka kushoto walioketi ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa (RAS) Wamoja Ayubu na Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mufindi Festo Mgina (Picha na Friday Simbaya)
Wajumbe
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa (RAS) Wamoja Ayubu akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao hicho.
Mkaguzi Mkuu wa nje w Hesabu za Serikali (Mkoa wa Iringa) Willy Joseph Undule akitoa ufafanuzi wa jambo leo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi cha kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa hesabu (CAG) zilizoishia tarehe 30 Juni, 2016. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Festo Mgina na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza.
MUFINDI: MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa kupata Hati safi ya Ukaguzi kwa hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2016.
alisema kuwa matokeo hayo ni ishara ya kazi nzuri iliyofanywa na madiwani kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri.
Hivyo, alitoa rai kwa halmashauri kuwa ushirikiano uliop uendelee kuimarishwa ili rasilimali za halmashauri ziendelee kutumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi... Endelea kufuatilia..
No comments:
Post a Comment