Monday, 7 August 2017

HAKIARDHI KUPIMA MASHAMBA 900 WILAYANI KILOLO


Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (HAKIARDHI) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa wakitialiana saini mkataba wa makubaliano ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji (VLUP) Ijumaa wilki iliyopita ambapo mashamba 900 katika vijiji vya Lukani, Ng’ang’ange na Mdeke wilayani humo vitapitiwa na mpango huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ernest Upemba, Mweneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Venance Kiwhanga, Afisa Programu wa HAKIARDHI Cathbert Tomitho na Mwanasheria wa Taasisi ya HAKIARDHI Joseph Chiombola. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Na Friday Simbaya, Kilolo

Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (HAKIARDHI) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa imepanga kupima mashamba 900 katika vijiji vitatu wilayani kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji (VLUP).

Katika mpango huo HAKIARDHI imepanga kupima vipande vya ardhi na mashamba 900 katika vijiji vitatu vya Lukani, Ng’ang’ange na Mdeke ambapo kila kijiji kitapimiwa mashamba 300 kupitia Programu ya Ardhi Yetu (AYP) kwa ufadhaili wa shirika la CARE International Tanzania.

Makabaliano hayo walitiwasaini Ijumaa wiki iliyopita na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ernest Upemba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo na Afisa Programu wa HAKIARDHI Cathbert Tomitho kwa upande wa HAKIARDHI.

Makataba wa makubaliano ulishuhudia na Mweneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Venance Kiwhanga kwa upande wa halmashauri ya kilolo na Mwanasheria wa Taasisi ya HAKIARDHI Joseph Chiombola.

Awali, Chiombola alisema kwa Mradi Mpya Wa Vijiji Vitatu umepanga kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji vipya 3, ambao utagharimu jumla ya shilingi milioni themanini na saba nukta nne (87.4m/-), hivyo kufanya jumla ya vijiji vilivyosapotiwa na HAKIARDHI kuwa 16. 

Vijiji hivyo ni Kihesamgagao, Kiwalamo, Kidabaga, Kipaduka, Ibofwe, Kitelewasi, Uhambingeto, Ilamba, Lugalo, Lyamko, Itonya na Vijiji vipya ni Ng’ang’ange, Mdeke na Lukani, Tayari utafiti wa awali wa kubainisha mahitaji ulishafanyika mwezi Julai 2017,

Alisema kuwa Matokeo ya utafiti yanaonesha vijiji hivyo vina changamoto kwa mfano, migogoro ya ardhi, hatari ya uhaba wa chakula, ukiukwaji haki za wanawake katika umiliki wa ardhi, na adhari ya mabadiliko ya tabianchi kupitia program ya ardhi yetu (AYP).

Chiombola alisema AYP ina malengo yafuatao; Kukuza uelewa wa wananchi juu ya masuala ya ardhi na ushiriki wao katika maamuzi yanayohusu ardhi na rasilimali vijijini, Kuimarisha vyombo vya utoaji maamuzi na haki juu ya ardhi katika serikali za mitaa (H/Kijiji, M/Kijiji).

Kuimarisha mikakati ya wananchi na viongozi wa serikali za mitaa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na Kuimarisha uwajibikaji wa serikali za mitaa kwa wananchi.

Naye mwakilishi kutoka tume ya taifa ya mipnago ya matumzi ya ardhi (NLUPC) Experancia Tibasama ametoa wito kwa halmashauri hiyo kuandaa wananchi hasa katika vijiji vinavyo husuka na mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji iliwaweze kushiriki kikamilifu.

Kwa upande wake Mweneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Venance Kiwhanga aliishukuru taasisi ya hakiardhi na wadau wengine wanaoshirikiana na taasisi hiyo kwa kuiwezesha halmashauri kupiga hatua katika utekelezaji wa sheria za ardhi na sheria za utatuzi wa migogoro.

Alisema kuwa halmashauri imeweza kuandaa hatimiliki zaidi ya 6700, kufundisha sheria ya ardhi ya vijiji Na.5 ya mwaka 1999 na sheria ya utatuzi wa migogoro ya mwaka 2002 kwa vijiji vyote.

Pia kupitia shughuli hizo ardhi wameshuhudia mwamko mkubwa wa wananchi hususani katika umilikaji wa ardhi, utawala na utatuzi wa migogoro.

“Tunafarijika sana kuona tunafanya uzinduzi wa mradi mwingine wa vijiji vitatu ambapo inatarajiwa kupima mashamba takribani 900, hakika tunawashukuru sana wadau wote…,” alisema Kiwhanga.

Alisema kuwa pamoja na mchango wa wadau mbalimbali kwenye masuala ya ardhi katika Wilaya ya Kilolo, bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazogusa jamii kama vile; mitazamo ya kijamii juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi, uuzaji holela wa ardhi kwa baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kilolo.

Hata hivyo, halmashauri ya wilaya ya kilolo, mkoani iringa inajumla ya vijiji 94 lakini vijiji 40 tu ambavyo vina mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji kwa mujibu wa afisa ardhi wa wilaya ya kilolo, Elinaza Kiswaga.

Mwisho







No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...