Sunday, 6 August 2017

MAKAMU W SHULE YA SEKONDARI POMERINI AANIKA SIRI YA MAFANIKIO


Makamu wa Shule ya Sekondari Pomerini wilayani kilolo, mkoani Iringa Allan Emmanuel Ngede ameanika siri ya kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, kwamba ni kutokana na sapoti ya wazazi, walimu, serikali ya kijiji na serikali kwa ujumla pamoja na wadau.

“Siri ya mafanikio ni umoja wetu kati ya wazazi, walimu, wanafunzi, serikali ya kijiji pamoja serikali kuu kwa kuweka viwango vinavyotakiwa katika kuboresha elimu nchini…,” alisisitiza makamuwa shule huyo.

Alisema kuwa shule ya Pomerini imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika ya shule 20 ambapo wanafunzi 53 wote wamefaulu na kupata sifa za kujiunga na vyuo, isipokuwa mwanafunzi mmoja tu ambaye amekosa sifa ya kujiunga na chuo kutokana na matatizo ya kinidhamu.

Ngede akiongea na Nipashe jana alisema kuwa wanafunzi wengi walifanya vizuri katika masomo ya history na kiingereza kuliko masomo ya jografia na Kiswahili.

Alisema kuwa katika matokeo hayo wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi sita, daraja la pili ni 43 wakati katika daraja la 3 ni wanafunzi wanne tu, lakini hakuna mwanafunzi aliopata daraja la nne.

Aidha, shule ya Sekondari Pomerini wilayani kilolo, ambayo ina milikiwa na Kanisa la KKKT imeshika nafasi ya 45 kitaifa kati ya shule 449.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...