Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ameweka wazi kuwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi hususan chakula yanazidi kushuka tofauti na tunavyonunua katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana kuingia kwenye uchumi wa viwanda.
Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika tathmini ya hali ya uchumi kwenye mauzo, na kusema kuwa anguko kubwa la mauzo tofauti na tunavyonunua, linatufanya kuzidi kuwa tegemezi.
“Uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje umeongezeka kwa 14% ndani ya mwaka mmoja wa Mei 2016 mpaka Mei 2017, ambapo Tanzania ilitumia dola 480 milioni kuagiza vyakula kama sukari, nafaka na mafuta ya mawese. Tumekuwa tegemezi zaidi, tunauza bidhaa kidogo zaidi nje ya nchi, na tunanunua bidhaa zaidi kutoka nje", aliandika Zitto Kabwe.
Mbunge Zitto Kabwe aliendelea kuandika kuwa pesa ambayo serikali inapoteza kwa anguko la mauzo ya bidhaa ndani ya miaka miwili ni nyingi, ambayo ingeweza hata kununua ndege 23 za aina ya bomberdier Q400
“Wakati Serikali inaimba viwanda, mauzo ya bidhaa zitokanazo na viwanda kwenda nje ya nchi yetu yameshuka sana, mwaka unaoishia Mei, 2016 Tanzania iliuza nje bidhaa za viwanda za thamani ya dola 1.5 bilioni.
Mwaka mmoja baadaye Tanzania imeuza nje bidhaa za viwanda za thamani ya dola 0.8 bilioni tu. Anguko la mauzo nje la takribani dola 700 milioni sawa na thamani ya Ndege 23 za Bombadier Q400", aliandika Zitto Kabwe.
No comments:
Post a Comment