Wakati Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), likitangaza rasmi kuanza kwa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), kesho Septemba 6 mwaka huu, kote nchini, wito umetolewa kwa wazazi kutobweteka badala yake waanze maandalizi ya watoto hapo baadaye.
Wito huyo umetolea na Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa (REO) Bw. Majuto Salehe Njanga wakati akiongea na gazeti la mwananchi katika mahojiano maalum leo.
Bw. Njanga alitoa wito kwa wazazi kuwa huu si wakati wa kubweteka na kujisahau na matokeo yake mnashtuka siku za mwisho mtoto ameshachaguliwa kwenda sekondari huku hamjafanya maandalizi.
“Kuanzia sasa wazazi na walezi, anzeni kujiwekea akiba kwa tahadhari ili watoto wenu watakapochaguliwa kuendelea na masomo, basi msione uzito wa kuwapeleka sekondari,” alisema Bw. njanga
Chonde chonde wazazi wenzangu, endapo mtaanza kujiwekea akiba kidogo kidogo ya kuwapeleka watoto wenu sekondari, ni dhahiri kuwa hamtakosa sare za shule, madaftari na ada, alisema afisa elimu huyo.
Wakati huouhuo, Afisa elimu wa Mkoa wa Iringa Bw. Majuto Salehe Njanga amesema mkoa wa iringa unajumla ya watahiniwa 24,906 ambao watafanya mtihani wa wa kuhtimu elimu ya msingi kwa mwaka 2017.
Alisema kuwa mitihani hiyo itaanza siku ya kesho ya tarehe 6 na itamalizika tarehe 7.
Aliseleza kuwa wasichana wanaotarajiwa kufanya mtihani huo ni 13,412 huku wavulana wakiwa 11,494 kwa shule zote mkoani iringa.
Aidha Bw. Njanga amewataka wanafunzi kuepuka udanganyifu kwa kupewa mitihani nje ya chumba cha mtihani.
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa shule zote za mkoani wanangoja kesho kuanza mitihani hiyo.
Wataniwa watakaofanya mitihani wa kumaliza elimu ya shule ya msingi kila wilaya ni kama ifuatavyo; manispaa ya iringa ni wanafunzi 3,738 (wasichana 1,976 na wavulana 1,762), wilaya ya iringa ni watahiniwa 6,519 (wasichana 3,493 na wavulana 3,026), Kilolo ni wanafunzi 5,940 (wasichana 3,221 na wavulana 2,719), Mufindi ni 6,820 (wasichana 3,724 na wavulana 3.096) na Mafinga mji ni jumla ya watahiniwa 1,889 (wasichana 998 na wavulana 891). Na Friday Simbaya, Iringa
No comments:
Post a Comment