Thursday, 16 November 2017

STEP WATOA VIFAA VYA DORIA KWA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILI UZUNGWA SCARP







Mkurugenzi wa shirika la Southern Tanzania Elephant Project (STEP) Dkt. Trevor Jones (kushoto) na Mhifadhi Mazingira Asili Uzungwa Scarp Mkiramweni Nzinyangwa wakibadilishana hati baada kusaini mkataba wa msaada wa vifaa vya doria uliyotolewa na STEP kwa ajili ya kusaidia kufanikisha doria katika hifadhi mazingira Asili ya Uzungwa jana. Anayeshuhudia ni Menja wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Florian Mkeya (picha na Friday Simbaya)


WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamepongeza shirika la Tanzania southern elephant project (STEP) kwa kutoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya doria kwa hifadhi ya uzungwa scarp ya mkoani iringa venye thamani ya shilingi milioni kumi (10m/-).

Meneja Misiti wa TFS kutoka makao makuu Dar es salaam Florian Mkeya, ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema hayo jana wakati akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya hifadhi ya mazingira asili uzungwa scarp (USNFR).

Alisema kuwa vifaa hivyo vitasadia kufanikisha doria katika hifadhi ya uzungwa, ikizingatia awali walikuwa wanafanya doria chache kutokana na ukosefu wa vifaa maalum kwa ajili ya doria.

Mkeya alisema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka wakati kumekuwepo na changamoto za uhifadhi katika hifadhi hiyo.

Alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na kamera, GIS, darubini, matulubai, viatu na vingine vingi.

Kwa upande wake, mkugerenzi wa shirika la STEP Dkt. Trevor Jones alisema kuna umuhimu wa kutunza hifadhi ya uzungwa kutokana na kuwepo kwa viumbe na wanayama adimu pamoja na vyanzo vya maji

Alisema kuwa vifaa hivyo wametoa kwa kushirikana na wadau mbalimbali kama vile whitley Wildlife conservation trust (UK) na Muse-Museum of natural science (Trento, Italy) Uhifadhi wa Uzungwa utasaidia pia kunusuru bonde la uhifadhi la kilombero mkoani Morogoro.

Alisema kuwa wanaendelea kutoa misaada katika hifadhi mbalimabli ikiwemo Hifadhi ya Mazingira ya Kilombero.





No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...