Na Friday Simbaya, Iringa
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Andy Karas ameridhishwa na utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wilayani Iringa kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini nchini kwa awamu ya tatu.
Karas alisema hayo jana walipotembea Kijiji cha Igingilanyi wilayani Iringa, mkoani Iringa na kujionea matokeo ya program mbalimbali zinazoendeshwa na USAID kama vile sekta ya kilomo, lishe, elimu,afya, wanawake na vijana na utawala bora.
Alisema kuwa amefurahishwa na hali za wanufaika kwa kuona baadhi ya wanufaika maisha yao yamebadilika kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufagaji wa kuku na nguruwe.
“Nimefurahi sana kuona baadhi ya wananchi wakibadilika kimaisha kwa kuwa na makazi bora kupitia msaada unaotelewa na USAID kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii kupitia mpango wake wa kunusuru kaya masikini,” alisema Karas.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Andy Karas alifanya ziara mkoani Iringa iliyoanza jumatatu hadi ijumaa wiki iliyopita kwa lenga la kujionea matokeo ya programu mbalimbali zinazoendeshwa na USAID mkoani humo pamoja na kufanya mazungumzo na wabia na walengwa wa programu hizo.
Alisema kuwa ziara hiyo inaakisi wigo mpana wa miradi inayofadhiliwa na Marekani nchini Tanzania, ikijumuisha sekta za kilimo, lishe, elimu, afya, wanawake na vijana na utawala bora.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge amelipngeza Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika kusaidia juhudi za serikali za kuwaondoa wananchi wanaokabiliwa na umasikini.
“TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi,” alisema Kamagenge.
Jumla ya kaya 97 za Kijiji cha Igingilanyi zinanufaika na mfuko wa maendeleo wa jamii kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo imeelezwa kuwa kaya hizo zimelipwa mara 14 na zaidi ya milioni 49 zimetolewa kwa wanufaika.
Hata hivyo, serikali imejipanga kuborsha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchini ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa na kuondoa malalamiko ya wananchi kuwa mpango huu umekuwa ni wa Kaya chache na fedha hizo utolewa kwa upendeleo.
No comments:
Post a Comment