Friday, 1 December 2017

WAZIRI WA NISHATI APIGA MARUFUKU KUNUNUA NGUZO NJE YA NCHI

















Waziri wa nishati Dkt. Medrad Kalemani amepiga marufuku uagizwaji wa nguzo za umeme na badala yake tanesco na rea waagize nguzo kutoka viwanda vya ndani.

Dkt kalemani alitoa agizo hizo hivi karibuni wakati wa ziara yake siku moja mkoani iringa.

Alisema makampuni ya ndani yanayozalisha nguzo yana uwezo mkubwa wakutosheleza mahitaji ya nguzo kwa tanesco na rea katika kutekeleza mradi wa umeme vijijni awamu ya tatu.


Akiwa mkoani hapa alitembelea viwanda vya Qwihaya General enterprises na sao hill industries vyote vya wilayani mufindi.

Alisema kuwa lengo ni kuunga mkono kaulimbiu ya rais dkt. john Pombe Magufuli ya tanzania yenye viwanda.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...