Na Friday Simbaya, Iringa
Familia ya mkazi mmoja wa Mwangata Msikitini katika kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa yanusurika kuteketea kwa moto baada ya majirani kuwaokoa kwa kufumua dirisha la nyuma ya nyumba yao.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5:30 asubuhi wakati famila ya onesmo cosmas ikiwa ndani wakiendelea na shughuli ambapo chanzo za moto kinadaiwa ni mtungi wa gesi kuvuja.
Mwandishi wa gazeti la Nipashe alishuhudia wananchi wakihangaika kuzima moto kwa kutumia mipira ya maji na ndoo pamoja na mchanga ambapo hatimaye uliwashinda na kuomba msaada kutoka jeshi la zimamoto.
Baadhi ya mashuhuda walioongea na Nipashe jana walisema kuwa wamepiga simu ya dharura ya zimamoto ambayo ni 114 kuwajulisha tukio la moto ambapo walisema gari la zimamoto na uokoaji lilifika kwa kuchelewa baada ya muda na kuudhibiti moto kabla haujashika nyumba nyingine za jirani
Shuhuda wa ajali ya moto Musa Juma ambaye ni mkazi wa Kata ya Mwangata alisema kuwa alisikia kelele za watu wakisema moto, moto ndipo alikurupuka na kwenda kuangalia na kusaidia kuzima moto.
Alisema kuwa majirani walipiga simu muda mrefu jeshi la zimamoto lakini lilifika kwa kuchelewa nakukuta banda lililoezekwa kwa nyasi limeteketea lakini walifanikiwa kuuzima kabla haujasambaa katika nyumba za mwambata ya familia Onesmo Cosmas.
Cosmas ambaye ameoa mzungu alikuwa hayupo wakati ajali ya moto inatokea alimuacha mke wake na watoto ndipo walitokea baada ya kupigiwa simu na mke wake. Mke wa Cosmas aligoma kuogea na vyombo vya habari vilivyofika kushuhudia tukio hilo la moto.
Majirani waliokoa familia ya bwana Cosmas kwa kufumua dirisha la nyuma ya nyumba yao na kuanza kuwatoa kupitia dirisha baada ya kushindwa kutokea mlango ambapo ilisadikika moto ulianzia mlangoni ya nyumba ya nyasi amabyo ilitumika kama sehemu ya kupumzikia wageni.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Iringa Mrakibu Msaidizi James Micheal John alidhibitisha kutokea kwa moto na kusema kuwa wamefanikiwa kuzima moto kabla haujaleta madhara.
Alisema kuwa walipigiwa simu na wananchi majira ya saa 5:30 asubuhi kwamba maeneo ya Mwangata msikitini inauungua moto na hatimaye kufanikiwa kuudhibiti moto kabla haujasambaa katika nyumba za mwambata za bawna Cosma pamoja na za majirani.FAMILIA YA MKAZI MMOJA WA MANISPAA YA IRINGA NUSURA ITKETEKE KWA MOTO
Na Friday Simbaya, Iringa
Familia ya mkazi mmoja wa Mwangata Msikitini katika kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa yanusurika kuteketea kwa moto baada ya majirani kuwaokoa kwa kufumua dirisha la nyuma ya nyumba yao.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5:30 asubuhi wakati famila ya onesmo cosmas ikiwa ndani wakiendelea na shughuli ambapo chanzo za moto kinadaiwa ni mtungi wa gesi kuvuja.
Mwandishi wa gazeti la Nipashe alishuhudia wananchi wakihangaika kuzima moto kwa kutumia mipira ya maji na ndoo pamoja na mchanga ambapo hatimaye uliwashinda na kuomba msaada kutoka jeshi la zimamoto.
Baadhi ya mashuhuda walioongea na Nipashe jana walisema kuwa wamepiga simu ya dharura ya zimamoto ambayo ni 114 kuwajulisha tukio la moto ambapo walisema gari la zimamoto na uokoaji lilifika kwa kuchelewa baada ya muda na kuudhibiti moto kabla haujashika nyumba nyingine za jirani
Shuhuda wa ajali ya moto Musa Juma ambaye ni mkazi wa Kata ya Mwangata alisema kuwa alisikia kelele za watu wakisema moto, moto ndipo alikurupuka na kwenda kuangalia na kusaidia kuzima moto.
Alisema kuwa majirani walipiga simu muda mrefu jeshi la zimamoto lakini lilifika kwa kuchelewa nakukuta banda lililoezekwa kwa nyasi limeteketea lakini walifanikiwa kuuzima kabla haujasambaa katika nyumba za mwambata ya familia Onesmo Cosmas.
Cosmas ambaye ameoa mzungu alikuwa hayupo wakati ajali ya moto inatokea alimuacha mke wake na watoto ndipo walitokea baada ya kupigiwa simu na mke wake. Mke wa Cosmas aligoma kuogea na vyombo vya habari vilivyofika kushuhudia tukio hilo la moto.
Majirani waliokoa familia ya bwana Cosmas kwa kufumua dirisha la nyuma ya nyumba yao na kuanza kuwatoa kupitia dirisha baada ya kushindwa kutokea mlango ambapo ilisadikika moto ulianzia mlangoni ya nyumba ya nyasi amabyo ilitumika kama sehemu ya kupumzikia wageni.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Iringa Mrakibu Msaidizi James Micheal John alidhibitisha kutokea kwa moto na kusema kuwa wamefanikiwa kuzima moto kabla haujaleta madhara.
Alisema kuwa walipigiwa simu na wananchi majira ya saa 5:30 asubuhi kwamba maeneo ya Mwangata msikitini inauungua moto na hatimaye kufanikiwa kuudhibiti moto kabla haujasambaa katika nyumba za mwambata za bawna Cosma pamoja na za majirani.
Mrakibu msadizi wa jeshi la zimamoto aliongeza kuwa nyumba iliyoungua haikuwa na umeme na kusema kuwa chanzo cha moto bado hakijafahamika ila moto unaonekana kama ulihama kutoka sehemu moja.
Kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi kuzingatia ramani za nyumba zao kwa kwenda Manispaa ili ramani hizo ziweze kuchunguzwa pamoja na kuangalia miuundombinu.
John Alisema miundombinu imekuwa kikwazo kikubwa kwa gari la zima moto kushindwa kufika eneo la tukio kwa kuchelewa.
Aidha, kamamda huyo waliomba pia wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la zimamoto kwa kupiga simu ya dhararu ambayo ni 114 bure na kuwaasa kuwaomba wasitumie namba hiyo kwa kutoa taarifa za uongo kwa sababu zitakwamisha juhudi za jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment