Monday, 19 February 2018

WILAYA YA KILOLO YATENGA HEKTA 72.3 KWA AJILI YA UWEKEZAJI


Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoor

Image may contain: 1 person, indoor

Kampeni ya uanzishaji wa viwanda kote wilayani Kilolo Mkoani Iringa imezinduliwa jana huku mwito zaidi ukielekezwa kwa umma kutoa ushirikiano kwa timu ya wataalamu katika kutekeleza mradi wa viwanda. 

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalla alisema eneo lenye ukibwa wa hekta 72.3 limetengwa kwa ajili ya viwanda huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo. 

Kampeni ya uanzishaji wa viwanda kote wilayani Kilolo Mkoani Iringa imezinduliwa huku mwito zaidi ukitolewa kwa wananchi kujiunga kwenye vikundi kujisajili na kutoa ushirikiano kwa timu ya wataalamu itakayochunga mwenendo wa viwanda vidogo. 

Abdalla alisema eneo lenye ukibwa wa hekta 72.3 limetengwa kwa ajili ya viwanda huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa zikiwamo za uchakataji wa mazao ya misitu na mashambani. 

Hadi sasa wilaya ya Kilolo inakadiliwa kuwa na viwanda 22 , Hatua hii ya uzinduzi inajiri baada ya 

Mkoa wa Iringa kuzindua mwishoni mwa mwaka uliopita kwa minajili ya utekelezaji wa agizo la 

Waziri wa Tamisemi seleman Jaffo la kutaka ifikapo baadae mwezi Disemba kila mkoa kuwa na viwanda 100. 

Asiah Abdalla anahimiza umoja kuelekea utelezaji wa azma ya serikali kuufikia uchumi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda. 

Mkuu wa wilaya anasema kulingana fursa zilizopo wilayani humo ikiwa mazao ya mashambani na misitu, shughuli za ujenzi kunauwezekano mkubwa wa kuanzisha viwanda. 

Baadhi ya wadau wakiwamo sekta ya fedha wanawaambia wajumbe wa kikao hiki muhimu kwa utekelezaji wa azma ya serikali ya kila mkoa lazima kuwe na viwanda mia moja kwamba mitaji si tatizo maadam wajisajiri tu. 

Mkutano wa wadauwa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi wilayani kilolo waliandaa kikao hicho kichoambatana na uzinduzi wa kampani ya ‘Wilaya yetu, Viwanda vyetu’ yakuchochea wananchi kushiriki kikamilifu kwa ujenzi wa uchumi wa viwanda. 


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...