Shirila lisilo la kiserekali la WorldShare toka Korea Kusini limeanza ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya sekondari Kidamali iliyopo katika kata ya Nzhi wilayani Iringa, mkoani Iringa ilikupunguza tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike.
Hayo yalifahamika jana wakati Mkuu wa Shule ya Sekondari Kidamali Sixtus Kanyama alipokuwa anatoa taarifa ya shule hiyo kwa maafisa toka ubalozi wa Korea Kusini na maafisa wa shirila la worldshare na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na tatizo la mimba kwa watoto wa kike kutokana na kutokuwepo hosteli ya wasichana ambapo wanafunzi wanalazimika kupanga vyumba mitaa na kukumabana na vishawishi mbalimbali.
Kanyama alisema kuwa Shule ya Sekondari Kidamali inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mimba kwa watoto wa kike kwa kuwa wingi wao wamepanga vyumba na kuishi pekee yao bila ulinzi.
Alisema kuwa wanafunzi wengi wanatembea umbali mkubwa kwenda shule na kuridi takriban kilometa 40 kila siku na kupelekea kuongezeka kwa utoro mkubwa na kutojihusisha na masomo.
Alisema kuwa kutokuwepo na hosteli kwa wanafunzi kumepelekea mdondoko kuwa mkubwa hasa kwa wanafunzi wa kike ambao husababishwa na vishawishi vya wanaume na kufanya mazingira ya shule kutovutia kuendelea na shule.
Aidha, Mwalimu Mkuu huyo alisema kuwa wanafunzi wengi wakiwemo wa kike wanajihusisha na makundi rika yenye tabia hatarishi na kuongeza kuwa wastani wa mimba 16 zinaripotiwa kila mwaka katika shule hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga ambaye aliambana na maafisa wa Ubalozi ya Korea Kusini na maafisa wa WorldShare, alilishukuru Shirika la Worldshare kwa kukubali kujenga bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kidamali.
Alisema kuwa hosteli ni jibu kwa matatizo hayo, kwa kuwa zipo faida nyingi za wanafunzi kukuishi bwenini na kuzitaja faida hizo kuwa ni pamoja na wanafunzi wa kike watakuwa alama kwa kuwa watakuwa chini ya matroni na walimu.
Dkt Mahiga alisema kuwa faida zingine kwamba wanafunzi watapata muda mwingi wa kujisomea, watapata malezi yanayofanana na kulindwa, wanafunzi wa kike wengi watafaulu na kujiunga na elimu ya juu.
Alisema kuwa hosteli inayotarajia kujengwa hapo shuleni itapewa jina la ‘Nara Memorial Dormitory’ ambapo ‘Nara’ kwa luhga ya kikorea ina maana ya nchi, Nara ni mwanzishi wa wazo la kujenga hosteli ya wasichana katika shule ya kidamali, lakini amekufa kabla wazo lake halijatimia.
Naye, Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Kidamali Emmi Mkupasi alilishukuru Shirika la Worldshare toka Korea Kusini pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt Mahiga kwa kuwatafuta wadau hao kuja kuwajengea hosteli ya wasichana.
Alisema kuwa uwepo wa hosteli ya wasichana kutasaidia kupunguza tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike kwa vile watoto wa kike wengi wanashinda kumaliza shule kutokana na changamoto nyingi ikiwemo tatizo la mimba.
Dada mkuu Mkupasi kutoka kidato cha cha tatu aliongeza kuwa wapo wanafunzi walioanza nao kidato cha kwanza lakini waliaacha shule kwa sababu ya mimba kwa vile wanafunzi wengi wamepanga vyumba mitaani.
Naye mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Robert Masunya ambaye aliongozana na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo akiwemo Diwani wa Kata ya Nzihi, Stephan Mhapa, alishukuru shirika hilola worldshare kutoka korea kusini.
Alisema kuwa shule ya kidamali ya sekondari inakabiliwa na changamoto ua ukosefu wa makataba, ukosefu wa ukumbi wa mikutano, maabara ya za masomo ya sayansi ambazo zipo lakini hazijamalika kujengwa na vyoo vilivyopo vyote matundu 16 ni chakavu.
Masunya alisema kuwa changamoto zingine ni nyumba za walimu, maabara ya TEHEMA, na kisima cha maji.
Hata hivyo, Shirika la WorldShare toka Korea kusini limekubali kujenga hosteli ya wasichana pamoja na kujenga fensi ya kuzunguka bweni hilo, kujenga vyoo na kuchimba visima vya maji ilikutatuwa tatizo la maji shuleni hapo.
Shule ya sekondari kidamali ni shule ya kata ambayo kwa kiasi kikubwa imejengwa kwa nguvu za wananchi. Shule iko taarifa ya kalenga, kata ya nzihi na kidamali.
Shule hii ilifunguliwa tarehe 30.05.2005 ikiwa na wanafunzi 76; wavulana 40 na wasichana 36, kwa sasa shule ina wanafunzi 600 kati yao wasichana 368 sawa na asilimia 61 na wavulana 232 sawa n asilimia 39 ya wanafunzi woyte.
Shule hiyo ina walimu wako 35, wakikie 15 na wakiume 20 na ina wa ekari 15.84. Shule ya sekondari kidamali inahudumia jumla ya vijiji vine ambavyo ni Kipera, Nyamihuu, Nzihi na kidamali. Na Friday Simbaya, Iringa
No comments:
Post a Comment