Saturday, 7 April 2018

NFRA YAJIPANGA UZINDUZI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA


Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Leo 6 Aprili 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-NFRA
Wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichoongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba, Leo 6 Aprili 2018.
Kutoka kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Fredy Mbonde, Afisa Ugavi NFRA Magreth Salia Kavishe, na Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichofanyika katika Ofisi za NFRA Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma, Leo 6 Aprili 2018
Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA na Mratibu wa Mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula, akiwasilisha maelezo mafupi ya namna mradi utakavyotekelezwa wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA, Leo 6 Aprili 2018
Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa maendeleo na Bishara wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Mikalu Mapunda (Kshoto), 


Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula katika dhifa itakayofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula zilizopo Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma.


Hayo yamebainishwa leo 6 Aprili 2018 na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma.


Bi Zikankuba ameeleza kuwa Mradi huo utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Aidha, amesisitiza kuwa mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi tarehe 9 Disemba 2017 huku akisema Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o) ambapo msimamizi wa utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Alisema Mradi utahusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa pamoja na ukarabati wa ofisi na kutekelezwa katika maeneo nane ambayo ni Arusha (Babati), Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Mpanda. 


Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa 250,000 MT zaidi (vihenge vya kisasa 190,000MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.


Alisema kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.


Hifadhi ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992 Wakala ulipoanzishwa.


Pia, technologia ya vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi, itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.


Katika kikao kazi hicho Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba amewasihi wafanyakazi wote wa NFRA kufanya kazi kwa ushirikiano na kutambua kuwa nidhamu na bidii yao itakuwa chachu ya mafanikio zaidi katika kuimarisha utendaji wa NFRA.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...