Monday, 11 June 2018

RITA WAANZA MAJARIBIO YA MPANGO WA VIFO MKOANI IRINGA



Na Friday Simbaya, Iringa 

Serikali kupitia wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja la Mafaita la kuhudumia watoto (UNICEF) na taasisi ya Bloomberg Data for Health pamoja na wadau maendeleo wengine imeanza kutekeleza mpango wa majaribio wa kusajili vifo mkoani Iringa. 

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson alisema hayo jana wakati wa kikao cha hamasa kwa viongozi wa mkoa na wilaya kuhusu majaribio ya mpango wa usajili wa vifo. 

Alisema kuwa kwa mara pili, Mkoa wa Iringa umepewa nafasi yakutekeleza mpango wa majaribio ya usajili wa vifo baada ya kufanya vizuri katika mpango wa maboresho ya mfumo wa usajili wa vizazi kwa watoto walio umri chini ya miaka mitano. 

Hudson alisema kuwa mkoa wa Iringa baada ya kufanya vizuri katika mpango wa maboresho ya mfumo wa usajili wa vizazi kwa kundi la watoto chini ya miaka mitano ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2016, umepewa nafasi tena nafasi ya kutekeleza majaribio ya vifo. 

“Tumefanikiwa katika vizazi, sasa hatuna budi kukamilisha hii jozi (pair). Tunanza majaribio kwa ajili ya kugatua majukumu ya usajili wa vifo hapa mkoani Iringa ambapo matokeo yatakayopatikana yatatumika kuboresha mfumo kabla ya kuanza kuenezwa nchi nzima, ” alisema Hudson. 

Kikao hicho pia kilishirikisha wada mbalimabli wakiwemo viongozi wa dini na wanahabari kama sehemu muhimu ya jamii. 

Alifafanua kuwa lengo la kuwashirikisha viongozi dini mbalimbali ni kwa vile vifo vititokea watu wanakimbilia kwenye nyumba za ibada. 

Alisema kuwa viongozi wa dini watawasaidia kutumia fursa walionazo katika kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kusajili matukio ya vifo. 

Tofauti na vizazi, kwa mujibu wa takwimu za vifo zaidi ya asilimia 85 vinavyotekea nyumbani wengi huzikwa bila kufika hospitali lakini hao wote huwawanishia kwa viongozi wa dini katika mazishi. 

Hudson aliongeza kuwa wanahabari kama sehemu ya jamii wananafasi kubwa ya kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii kuhusu usajili wa vifo, hivyo basi, wanombwa ushirikiano katika mfumo huo wa usajili wa vifo. 

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho cha hamasa aliwapongeza RITA katika mageuzi wanayoendelea kuyatekeleza katika maeneo mbalimbali nchini. 

Alisema kuwa taasisi nyingi zina mengi ya kujifunza hasa katika suala la kusogeza huduma karibu na makazi ya wananchi kwa kugatua madaraka. 

Alisema kuwa kifo ni tukio linalosababisha huzuni kwa sababu hutenganisha na wale tunowapenda ikimanisha hatutaweza kuwa nao tena katika maisha, pamoja hali hiyo, ni muhimu kuandikisha tukio hilo ili kupata cheti cha kifo ambacho kinatumika kama uthibisho wa kisheria wa kifo, aliongeza. 

Masenza alisema kuwa woga wa kifo walionao wananchi unaenda mbele zaidi kusababisha wengi kutosajili matukio ya vifo na kufanya nchi kuwa na wastani wa asilimia 17.5 ya vifo vinavyosajiliwa. 

Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuona uhusiano kati ya kusajili kifo cha ndugu yao na maendeleo ya nchi ili serikali iwezekupanga mipango yake ya maendeleo. 

“Nafahamu zipo nchi ambazo walishaacha kufanya sense kama tunavyofanya kila baada ya miaka kumi na kutumia fedha nyingi kwani nchi hizo wameweka utaratibu ambapo kila mtoto anayezaliwa anasajiliwa na kila mtu anayefariki anasajiliwa hivyo kuwa na takwimu za wananchi wake kila siku,” alsema masenza. 

Aidha, mkuu wa mkoa huyo alitoa rai kwa RITA kutoa fursa ya kuwaeleimisha viongozi wa mikoa umuhimu wa kuandika wosia na kwamba sio uchuro bali ni kwa faida ya familia watakayoiacha mara watakapoondoka duniani. 

Hata hivyo, masenza waliwataka viongozi wa mkoa na wilaya, viongozi wa dini, wanahabari, wadau wa maendeleo na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kutekeleza majario ya mpango wa usajili vifo. 


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...