Na Friday Simbaya, Iringa
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limewakamata watu saba wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio mbalimbali mkoani hapa kwa kukamatwa na vitu mbalimbali zikiwemo noti bandia dola za kimarekani pamoja na madini bandia.
Akizungumza na wanahabari mjini Iringa leo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire Makanya alisema kuwa wamemkamata mtuhumiwa Emmanuel Mtweve , 41, mfanyabiashara mkazi wa Tabata wa jijini Dar es Salaamu akiwa na noti bandia 63 mfano wa dola za kimarekani.
ACP Bwire alisema mtuhumiwa huyo Mtweve pia alikamatwa akiwa na madini bandia mithili ya dhahabu yenye uzito wa kilogramu 3.5 baada ya kufanyia upekuzi ndani ya gari yake keneye namba za usajili T 419 DLL aina ya Brevis.
Alisema kuwa katika swala la ufuatiliaji wamekamata wahusika wengine wanatuhumiwa kujihusisha na matukio mbalimbali akiwemo Abdallah Mohamed,43, mkulima na mkazi wa Madoto Mburahati, Abukakari Mwamedi, 40, mkazi wa Mbarali Mbeya, Seif Seleman,37, mkazi wa Chanika, Christopher Mgie, 37, Frank Lutanile na Abuu Mbinga wote wakazi wa Itamba Mbarali, mkoani Mbeya.
Vitu mbalimbali walivyokamatwa navyo ni mabunda matano ya makaratasi ya mfano wa fedha, sanduku la kienyeji la kubebea vitu hivyo, simu 19 za aina mbalimali za kuwapigia kwa ajili ya kutapeli, hirizi tano, rubber band za kufungia noti bandia na kilo nne za madini bandia mithili za dhahabu.
Aidha, jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa makini na kutokaa taarifa juu ya watu wa aina hiyo.
Katika hatua nyingine, jeshi la polisi mkoani Iringa linawatafuta watu sita (6) wanaosidikikiwa ni majambazi kwa kuvamia Fuad Faraji Abri,25, mkazi wa Wilolesi manispaa ya Iringa na kmpiga risasi kwenye paja la mguu wa kushoto.
ACP Bwire alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 13/07/2018 katikamaeneo ya Wilolesi Kata ya Gangilonga Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa.
Alisema kuwa majabazi hao alimvamia nyumbani kwake na watu siata walijificha nyuso zao kwa vikoi vya kimasai ambao waliruka uzio wa nyumba kwa kutumia ngazi mbili na kumteka mlinzi kwa kumfunga kamba mikononi kisha kuvunja mlango wa nyumba kwa nia kupora mali.
Kamanda Bwire alifafanua kuwa majabazi hao walifyatua risasi mbili za bastola ambazo zilimujeruhi Abri kwenye paja la mguu wa kushoto kitendo kilicholeta majibizano ya risasi pande mbili na kupelekea majambazi kukimbia kutoka eneo la tukio.
Hata hivyo, watuhumiwa wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo la kunyang’anya kwa kutumia silaha na msako bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment