Monday, 1 November 2010

NDONDOO ZA UCHAGUZI MKUU JIMBO LA LUDEWA-IRINGA

Jimbo la Ludewa (Mkoa wa Iringa) lilikuwa na jumla ya wapiga kura walioandikishwa 60,976 sawa na asilimia 80 ya lengo la uandikishaji (75,826), Msimamizi wa Uchaguzi Hildah Lauo ameeleza.

 Msimamizi wa uchaguzi huyo ambaye pia ni Mkurungezi wa Halmashauri ya Ludewa Jimbo la Ludewa lilkuwa na idadi ya vituo vya kupigia kura 202 yenye jumla ya kata 25, ambapo kata 14 kati  ya 25 zilipita bila kupingwa na kata kumi na moja (11) ndizo uchagazi wa madiwani ulifanyika na tayara kata ya Lupingu imenyankiliwa na upinzani (TLP).

Aidha, alisema kuwa matokeo ya awali katika uchaguzi wa urais kutoka kata nne (Ibumi, Iwela, mkomang'ombe na Luana)sawa na vituo vya kupgia kura 33 matokeo ya awali ya urais yakuwa, kura 3,992 walichukua CCM na CHADEMA walipata 1,414.

Alisema kuwa pamoja na idadi hiyo ya wapiga kura wa jimbo hili wananchi hawakujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu 2010 kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za kupoteza shada za kupigia kura na wengine kuamua kutopiga kura kabisa.

Kwa ujumla zoezi la upingaji kura katika Jimbo la Ludewa lilikwenda vizuri ambapo hakuna sehemu yoyote kulikoripotiwa kuwa na vurugu za kisiasa mpaka sasa.

Hata hivyo mchana huo tapata matokeo kamili kutoka kata zilizobaki zenye idadi ya wapiga kura wengi kama Mlangali na Lugalawa.

 Ok bye see you later, mchana mwema.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...