Peramiho
Timu ya wafanyakazi wa misioni ya Abasia Peramiho imeichapa Timu ya watumishi wa serikali mabao 4-2 Jumapili katika mashindano ya Mei Mosi 2011, yaliyofanyika katika viwanja vya Peramiho misioni, yakiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, wilayani Songea vijijini mkoani Ruvuma.
Katika mechi hiyo kipindi cha kwanza timu zote mbili ziliaanza kwa kushambuliana, ambapo timu ya Peramiho Misioni walifanikwa kupata magoli mawili ya chapuchapu ambapo timu ya watumishi wa serikali hawakupata chochote hadi kipindi cha kwanza kimalizika.
Kipindi cha pili kilipoanza timu ya watumishi iliaamka kutoka usingizini na kushumbulia lango la abasia ya Peramiho bila mafanikio na matokeo yake kuaacha mwanya kwa timu ya Abasia kuongeza magoli mengine mawili.
Timu ya Abasia walibweteka na ushindi wa magoli manne na kuwadharau ndipo timu ya watumishi walicheza kufa na kupona na kurudisha magoli mawili dakika za mwisho na mpira kumaliza kwa matokeo 4-2, ambapo timu ya Abasia walitoka kifua mbele na zawadi ya shilingi 50,000/=.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama alikuwa nidiye mgeni rasmi na mfadhili wa mashindano hayo ya Mei Mosi 2011, alishukuru timu zote mbili kwa kujitokezana kucheza vizuri bila ugomvi.
Wageni wengine walioambatana na mbunge huyo ni pamoja na Diwani wa Peramiho Izack Mwimba, wenyeviti wa vijiji vya Peramiho ‘A’ na Peramiho ‘B’ na watendaji wa vijiji hivyo.
Mbunge huyo ambaye ndiye mfadhili wa mashindano yaliyoshirikisha timu za soka za wafanyakazi wa misioni na watumishi wa serikali na kukabidhi zawadi ya shilingi hamsini taslimu (50,000/=) kwa timu wa Abasia Peramiho na timu ya watumishi wa serikali nao waliambulia shilingi 30,000/=.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Abasia iliibuka na ushindi wa mezani baada ya timu ya watumishi wa serikali kushindwa kufika kiwanjani, na kupatiwa zawadi ya shilingi 50,000/-.
Aidha, mbunge huyo wa Peramiho alielezea kupungua kwa zawadi kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana kuelekeza nguvu kwa timu ya soka ya Wilaya ya Songea vijijini daraja la kwanza itakayo wakilisha mashindano ya ligi ya daraja.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (katikati) akifantilia mashindano ya Mei Mosi kwa makini akiambatana na Diwani wa Peramiho, Izack Mwimba (wa kwamza kushoto)
Timu ya wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho ya wanawake upande mpira wa pete.
Mbunge Jenista Mhagama akisalimia Timu ya watumishi wa serikali kabla mechi kuanza katika viwanja vya Peramiho.
Mpira wa kona katika lango la Timu ya Peramiho wenye jezi ya mistali mweupe na golikipa wao mwenye tracksuit ya rangi damu ya mzee.
Kiongozi wa Timu ya Abasia (Netiboli) akipekea zawadi kutoka kwa mbunge Jenista Mhgama wa pili kutoka kulia.
Timu ya watumishi wa serikali wakipata zawadi ya shilingi 30,000/= kama mshindi wa pili katika mchezo wa soka.
Mabingwa wa mashindina ya Mei Mosi 2011 ambao ni Timu ya Abasia ya Peramiho wa kupita zawadi ya 50,000/= kutoka kwa mbunge, ikiwakirishwa na kepteni timu mwenye t-shirt ya bendera ya Marekani na begi mgongoni.
Timu ya wafanyakazi wa Abasia Peramiho katika picha ya pamoja kwa mechi.
Timu ya soka ya watumishi wa umma katika picha ya pamoja kwa kabla ya mechi.
No comments:
Post a Comment