MKAMATE elimu usimwache aende zake maana yeye ni uzima wako, na kama unadhani elimu ni gharama basi, jaribu ujinga. Hiyo ni kauli mbiu iliyotumika jana katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari ya Matakatifu Alois inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, Parokia ya Ludewa.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Georgina Bundala kama mgeni rasmi akiwakilishwa na Afisa Maaendeleo ya Jamii Wilaya Bw. Lazaro Mapunda aliongoza harambee hiyo iliyohudhuriwa na wadau na wananchi wachache lakini akafanikiwa kuchangisha jumla na zaidi ya shilingi 5m/- na kuungwa mkono na wageni kutoka makao makuu ya Jimbo Katoliki la Njombe.
Wananchi wilayani Ludewa wanatakiwa kushiriki na kuwekeza zaidi katika elimu ili kuongeza idadi ya wataalamu wilayani humo na Taifa kwa ujumla badala ya kupoteza muda na fedha nyingi kwenye vikao vya harusi na sherehe zingine zinazohusiana na mambo ya burudani,kuselebuka, kulakula na kunywa huku watoto wakiendelea kufanya vibaya katika mitihani yao.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi Georgina Bundala kwenye Ukumbi wa Kanisa Katoliki la Yesu Kristo Mkombozi Parokia ya Ludewa katika harambee maalumu ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Mtakatifu Alois inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Mdonga nje kidogo ya Mji wa Ludewa.
Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Paroko wa Parokia ya Ludewa Fr. Ladislaus Mgaya alisema kuanzishwa kwa shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki, Jimbo la Njombe kunatokana na tamko la Askofu wa Jimbo Alfred Maluma la mwaka 2003, lilinukuliwa kwenye Kitabu cha Mithali Sura ya 22 aya ya sita inayosema (mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha hata akiwa mzee).
Fr. Ladislaus Mgaya alisema Elimu na Malezi bora. Huu ndio wimbo tutakao kuwa tunaimba na kugharamia elimu, tamko hili lilianza kutekelezwa mwaka 2004 na Ludewa likaanza kuzaa matunda mwaka 2007 ambapo majengo yalianza kujengwa kwa nguvu za waumini wenyewe.
Fr. Mgaya alizitaja Changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na ujenzi wa maabara na nyumba tatu za walimu vyote vikiwa na thamani ya shilingi 50m/- na kwamba kwa sasa idadi ya wanafunzi shuleni hapo ni 98 wakiwemo wasichana 35 tu.
Naye Mkurugenzi wa elimu katika Jimbo Katoliki la Njombe, Fr. Bruno Henjewele aliwataka waumini na wananchi wote wa Ludewa kutofanya uzembe katika suala la elimu kwani badaye wanaweza kuja kupata majuto yenye maumivu makali kwani dunia ya leo bila elimu ni aibu kwa sababu hata vibarua wa kufagia atatakiwa kuwa na vyeti vya sekondari.
Wageni waliomwakilisha Baba Askofu katika Harambee hiyo ni pamoja na Fr Alexanda Mlelwa ambaye ni Paroko wa Parokia ya Makete na Mwenyekiti wa Mapadre wazawa Jimbo la Njombe, Fr Bruno Henjewele Mkurugenzi wa Elimu Jimbo, Mkuu wa Shule ya Msingi SICRED waliochangia shilingi laki tano, Shule ya Msingi Bakita waliochangia laki mbili na nusu.
Wengine Mkuu wa Shule ya Sekondri ya Ilowola waliochngia shilingi laki nne, Masista wa shule ya Mtakatifu Monica Seminari ya wasichana walichangia shilingi laki mbili, Shule ya Sekondari wavulana (Umawanjo) inayotegemea kujengwa Upangwa Bonde la Ludewa Lugarawa chini ya umoja wa mapadre nayo ilitoa shilingi laki moja sitini elfu taslimu.
Jimbo Katoliki la Njombe hadi sasa limefanikiwa kujenga shule nyingi zikiwemo za msingi na sekondari.
Mji wa Ludewa Pamoja na kuwa na makanisa Lukuki yanayoibukia kila kukicha kwa kuhubiri neno la Mungu ni Kanisa moja tu la Kianglikana ndilo lililoshiriki vyema harambee hiyo kwa moyo na kuchangia shilingi laki moja chini ya Mchungaji wake Padre Mtweve ambaye kwa upande wake aliwasihi wachungaji wenzake, na wananchi kwa ujumla kuwa waache kushiriki kwenye mialiko yenye kula waache tofauti za imani na kushiriki katika mambo ya msingi kama elimu kwani hata maandiko matakatifu yanaelekeza hivyo.
Elimu ni Sarakasi na kujenga shule moja ni sawa na kujenga makanisa mengi.Hiyo ilikuwa kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya walei Parokia ya Ludewa Bw. Linus Njalla Ngalomba alipokuwa akihitimisha harambee hiyo kwa kuwashukuru wale wote waliofanikisha zoezi hilo sambamba na wageini kutoka Jimboni Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment