Mkuu wa Mkoa wa Iringa ametoa mchango wa mabati 371 kwa
halmashauri za wilaya ya Iringa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara kwa
baadhi ya shule za serikali za kata.
Mchango huo ulikabidhiwa
na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Juma Masenza kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa,
Leticia Warioba katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja
vya ofisi ya mkuu wa mkoa leo.
Wilaya ya Iringa ina
halmashauri mbili ambazo ni Halmashauriya Manispaa ya Iringa na halmashauri ya Wilaya
ya Iringa.
Masenza alisema kuwa
mchango huo ni kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika ujenzi wa maabara
kwenye shule za serikali za kata utakaosaidia wanafunzi wengi kupenda masomo ya
sayansi na baadaye kuzalisha wataalamu wengi zaidi nchini.
Alisema kuwa kukosekana
kwa maabara katika shule nyingi za serikali kunasababisha wanafunzi wengi hasa
watoto wakike kuogopa kuchukua masomo ya sayansi.
Aidha, halmashauri
zilizonufaika msaada huo mabati ni pamoja na Manispaa ya Iringa na Wilaya Iringa.
Awali, Katibu Tawala wa
Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayub alisema kuwa Mkoa wa Iringa unahitaji jumla ya maabara
318 kwa shule 106 za sekondari mkoani, ambapo maabara zilizopo kwa sasa ni 48
tu.
Alisema kuwa ujenzi wa
maabara katika sehemu nyingi zipo katika
hatua mbalimbali za ujenzi na kuwaomba wadau zaidi wajitokeze kusaidia juhudi
ya serikali ya kujenga maabara zaidi.
Alisema kuwa mkuu wa
mkoa kwa niaba ya ofisi ya mkuu wa mkoa iringa alikabdhi mabati 180 kwa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mabati zingine 192 yalikabidhiwa kwa Halmashauri
ya Wilaya ya Iringa, zenye geji ya 28.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Leticia warioba akipokea mabati kwa niaba ya wakurugenzi wa
halmashauri hizo alimshukuru mkuu wa mkoa wa Iringa kwa juhudi yakufanyikisha ujenzi wa maabara kwa shule hizo za wilaya.
No comments:
Post a Comment