Monday, 8 December 2014

Airtel yazindua HOME Wi-Fi, huduma ya Internet kuunganisha familia nzima kwa kifurushi kimoja tu


Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa umakini uzinduzi  wa huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wa AIRTEL  watumiaji wa INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia,  na pia kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini.



Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  wa huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi kwenye  smartdevices 32 ndani ya familia na pia kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania  kufurahia internet ya 3.75G.  kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra.


Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia na wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania  kufurahia internet ya 3.75G.  Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando na kushoto ni Ofisa Masoko wa Airtel Tanzania,Ndevonaeli Eliakimu.


  • Zaidi ya  vifaa  32 kuunganishwa na  Wi-Fi ya nyumbani kwa kutumia kifurushi kimoja tu
  • Pia Simu za mkononi 4 zilizo mahali popote nchini kuunganishwa kwenye WiFi ya nyumbani hiyo hiyo
  • Ofa kabambe hadi ya GB 120  kutoleawa kwa bei nafuu

Airtel Tanzania leo imezundia huduma ya kwanza ya kibunifu nchini ijulikanayo kama “Home WiFi with bundle share” (WiFi ya nyumbani na kufurushi cha pamoja) itakayowawezesha watanzania na wateja wa Airtel kupata huduma ya Wi-Fi na kuunganisha zaidi ya vifaa vingine 32 vitakavyotumia WiFi .

Huduma hii vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G.  hii inamaanisha kifurushi cha internet kilichopo kwenye kifaa cha WiFI ya nyumbani  sasa kitakuwa na matumizi mawili yaani Wifi ya nyumbani na internet kwenye simu za mkononi pindi mteja akiwa  nje ya nyumbani

kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intenet kwa kila simu ,kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye WiFi ya nyumbani na kuwawezesha kila aliyeunganishwa na kifaa hicho kupata kifurushi chake kulingana na gawiwo alilowekea na hivyo kutumia kifurushi kimoja

ili kujipatia kifaa hichi cha HOME WiFi unaweza ukalipia : shilingi 195,000/-  na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 40 GB  kwa mwenzi au unaweza kulipia shilingi 250,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 120 GB  kwa mienzi mitatu, Aina zote mbili za ofa zinatoa huduma ya kutumia kifurushi kimoja na kuunganisha wanafamilia wanne wenye simu za mkononi ya malipo ya awali (prepaid line)

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja masoko na bidhaa hii wa Airtel Bw, Guarav Dhingra alisema” Dunia inabadilika na kukua kwa kasi ndivyo ilivyo kwa matumizi ya internet, kwa sasa internet si kwa ajili ya baba na mama, bali ni muhimu kwa familia nzima ikiwa ni pamoja na watoto kwaajii ya burudani, masomo,  na nyingine nyingi.  Ongezeko kubwa la simu za kisasa, komputa ndogo, Television za Kisasa, saa za kisasa, tablet katika nyumba zetu ni ushahidi tosha wa hili.

Wakati ongezeko na upatikanaji wa vifaa hivi ukiwa rahisi,  njia za kuunganiswa na huduma za internet zinazidi kuwa ngumu kwa wateja,  kwani inamgharimu mteja kuwa na simcard kwa kila kifaa, na kila simcard inabidi kusajiliwa na kuwekewa muda wa maongezi wakutosha , kisha kuingiza namba maalumu na kuchangua kirufushi na ndipo kuanza matumizi.

Airtel kwa kuona hii changamoto imekuja na huduma ya WiFi ambapo sasa unaweza kuunganisha vifaa hivi vyote kupitia kifaa cha WiFi cha nyumbani  na kupata intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada.  Na tumewawezesha wanafamilia kuweza kuongeza kifurushi cha intenet kwa kupiga *148*20# na kuunganishwa na kifurushi kimoja

Tunaamini familia nyingi zaidi nchini Tanzania watafurahia na kutumia huduma hii ya pekee toka Airtel na hivyo kutuamasisha kuongeza huduma nyingi za kibunifu za  internet” aliongeza Guarav Dhingra

Huduma hii inapatikana kwa kupiga 0784104800 ambapo utaweka oda yako kwajili ya kupata kifaa hiki cha  WiFi ya nyumbani, na  kisha Airtel itakuletea mahali ulipo na kukunganisha na huduma hii.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...