Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Frederick Mwakalebela ambaye pia ni Kamanda wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Iringa Mjini leo ametangaza nia kugombea tena ubunge kwa mara ya pili baada ya mwaka 2010 kutoswa na chama chaka licha ya kuongozi katika kura za maoni na nafasi hiyo kupewa kwa mshindi wa pili kura za maoni Monica Mbega na Chadema kushinda uchaguzi huo kupitia mgombea wa chama hicho wakati ule Mch. Peter Msigwa. Mwakalebela ametoa wito kwa watia nia wenzake kupitika ticketi ya CCM kuachana na siasa za kupakana matope na badala yake wafanye siasa za kistaarabu kwa ustawi wa chama. (Picha na Friday Simbaya)
RAIS WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA ADDO NOVEMBER MWASONGWE ATANGAZA NIA NA KUCHUKUWA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE IRINGA MJINI KWA TIKETI YA CCM.
Ndugu wanahabari leo tarehe 15.07.2015 nimekuiteni kuwaeleza juu ya Nia yangu ya kugombea Ubunge Iringa Mjini kwa ticket ya CCM. Sababu ninayo Nia ninayo na uwezo ninao kwa wananchi wangu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla. Natambua ya kua uongozi ni Mzigo.
No comments:
Post a Comment