Friday, 8 July 2011

MSIMU WA MAVUNO HUU HAPA












Msimu wa mavuno umewadia tena. Hawa ni wakazi wa  Mtaa wa Yerusalemu Peramiho, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma wakisaidiana kupukuchua mahindi baada ya mavuno kwa kutumia mashine ndogo inayosukumwa kwa nguvu ya genareta. Mashine hiyo ya kupukuchulia hukodishwa na wafanyabiashara kwa wakulima wadogo wadogo katika kipindi hiki cha mavuno. Mkoa wa Ruvuma ni maarufu sana kwa Kilimo cha mahindi. Hogereni sana kwa mavuno!

Sunday, 26 June 2011

MWENYEKITI TLP SONGEA AFARIKI DUNIA


Na Friday Simbaya,
S ongea
PAROKO Padre Joseph Ndimbo wa Parokia ya Peramiho Jimbo Kuu la Songea aliwaasa  waombolezaji kuacha mara moja tabia kugombeana maeneo ya kuzika marehemu.
Alisema kuwa kuna mtindo umezuka wanandugu kuvutana wapi wamzike marehemu na kuongeza kuwa huku ni kumdhalilisha marehemu.
Pd. Ndimbo alisema hayo Jumamosi wakati wa mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Tanzania labour Party (TLP)wilaya ya Songea, Bw. Kalo Kombe katika makaburi ya Liangano karibu na Kijiji cha Lipinyapinya Kata ya Peramiho.
Alisema kuwa sio tabia nzuri kwa wanandugu kugombeana maiti , kumbe maeneo yote yanafaa kuzikia.
“Imezuka tabia katika jamii ya watu kugombania maiti yaani mvutanao wa watu wawili kugombania maiti wakati wa  mazishi kila mtu anataka kuzika mahali pake, huku kote ni kuhangaika na kumtesa marehemu. Kuzikwa ni kuzikwa tu hata kama atazikwa Peramiho ‘A’ au Peramiho ‘B’,” alitoa mfano paroko huyu.
Aidha, paroko alisisitiza kuwa watu wasitafute mchawi kwamba marehemu amerogwa bali waendelee kumuonbea marehemu kuwa astarehe kwa amani kwa Mungu Baba.
Aliwaambia waombolezaji kuwa kuumwa kwa mwanadamu ni mateso kwa sababu mtu yeyote atakayependa maisha lazima afe lakini anayechukia maisha ataishi maisha ya milele.
Aliongeza kuwa WaTanzania vilevile tunakiwa  kufanya kazi kwa bidii sio kutafuta kwa njia ya mkato. Alisema kuwa mtu lazima apate mateso ili afe kama vile mtu anatakiwa kuteseka ili apate chakula. Aliongeza kuwa mateso ni sehemu ya maisha ya binadamu, kwa hiyo mtu akiuugua ni mateso, vilevile mtu kuchapakazi kwa bidii ni mateso pia ili kuweza kuishi maisha bora.
“Hakuna maisha bora kama hujishughulishi kwa sababu maisha bora huja kwa kufanyakazi kwa bidii na kuaacha uvivu,” alisema paroko. “Asiyefanya kazi na asile huo ndio wito wangu kwenu” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo wa TLP  alifariki dunia juzi katika hospitali ya Misioni ya St. Joseph Peramiho baada ya kuugua vidonda vya tumbo kwa muda mrefu.
Marehemu Kombe alistaafu katika Jeshi la Polisi tangu 1995, ambapo alifikia renki ya inspector kabla ya kustaafu na kuanza kujishughulisha na mambo ya siasa. Marehemu Kombe alipenda magauzi ndiyo maana alijiunga na upinzani, alikuwa anaishi maeneo ya Mjimwema katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Monday, 20 June 2011

MTOTO ANUSURIKA KUUNGUA MOTO


Mafundi wakiendelea na ukrabati wa nyumba iliyoteketea kwa moto hivi karibuni maeneo ya Peramiho, ambapo mtoto mdogo anayesoma shule ya chekechea alinusurika kuungua moto na baadae kuokolewa na wasamaria wema kwa kubomoa mlango kwa shoka. Mtoto huyo mara baada ya kuokolewa alikimbizwa katika hospitali ya Peramiho kwa uchunguzi zaidi, baada kubugia moshi mwingi. Mashuhuda waliongea na mwandishi walisema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyosababishwa na jiko la umeme lililoaachwa bila uwanagalizi. Aidha, familia mbili ambazo zilikuwa zikiishi katika nyumba hiyo kwa sasa zinajistili kwa majirani kwa muda huu huku wakisubiri kumalizika kwa ukarabati wa nyumba kwa kwekuweka bati badala ya vigae vilivyokuwa hapo mwanzo.




Fundi mmoja  akitoa mabaki  mbalimbali ya vyombo vya ndani kutoka chumba kulichonzia kuungua moto.


Sunday, 19 June 2011

ZAMBIA'S FIRST ELECTED PRESIDENT CHILUBA DIES







Frederick Chiluba pictured above, Zambia's first democratically elected president, has died at home at the age of 68.
Mr Chiluba was hailed as Zambia's "liberator" by his supporters when he came to office in 1991 after 27 years of single party Socialist rule.
He won praise for his economic and political reforms but was later accused of embezzlement and turning a blind eye to corruption.
The cause of his death is not known but he was known to have heart problems.
Under Mr Chiluba, Zambia was considered to be a model of African democracy and his presidency was welcomed in the West.
The former trade union leader and son of a copper miner introduced many reforms which dismantled the restrictive policies of former President Kenneth Kaunda.
But he was dogged by corruption allegations and was accused of taking an authoritarian approach to his political opponents, firing critical colleagues and jailing outspoken journalists.
He attempted to alter the constitution to allow him to run for a third term in office in 2001, but stood down after huge public protests.
Mr Chiluba was prosecuted for alleged embezzlement in 2002 but acquitted after a six-year trial.
In 2007, he was convicted of fraud by a London court and ordered to repay $58m in embezzled funds, but the ruling was never carried out by Zambia.
He spent his final years at his residence in Lusaka, confined by ill health and the confiscation of his passport by the authorities.
18 June 2011Last updated at 07:19 GMT
Frederick Chiluba, Zambia's first elected President
Frederick Chiluba came to power as Zambia's second president by defeating the once-revered Kenneth Kaunda in the first contested elections in the country for more than 20 years.
Democracy flourished during his 10-year rule, but the dapper and diminutive politician ended his career under a shadow of corruption.
He was the son of a copper miner, and was born in Kitwe, in what was then the British Protectorate of Northern Rhodesia.
Working as a clerk as a young man, he joined a building and engineering workers union, and visited East Germany and the Soviet Union, but later became disenchanted with Communist ideology. He rose through the union ranks to become chairman in 1971, and became increasingly involved in politics in Zambia.
He had been a supporter of Kaunda through independence in 1964, but became disillusioned with one-party rule, and in 1980 threatened to call a strike against the regime.
Widespread support
After months of turmoil, Kaunda ordered the arrest of Chiluba and three other union leaders, and they were held for three months, until a court ruled that their imprisonment was unlawful.
On his release Chiluba began to attract increasing support, and, in 1990, formed the Movement for Multi-Party Democracy, MMD, to oppose Kaunda's authoritarian rule.
With a bankrupt economy - foreign debt stood at more than $6.4bn (£4bn) - high unemployment and 100% inflation, he attracted widespread backing for his demands for economic reform and improved human rights.
Kenneth Kaunda relinquished power in 1991
Only five feet tall, he was nevertheless an impressive figure who, as a born-again Christian, brought the passion of the pulpit to his oratory.
President Kaunda finally bowed to demands for free elections which were held in November 1991 and closely assessed by 2,000 local and foreign monitors, including a Commonwealth team and one led by US ex-President Jimmy Carter.
The poll was declared free and fair, and Chiluba and his party were swept to power with more than 80% of the vote.
Kaunda stepped down in what was regarded as the most democratic change of government ever seen in Africa.
Chiluba inherited enormous economic problems, aggravated by the worst drought in the country for 50 years. He set about trying to persuade the West to come to his aid in setting up a free-market economy, and promised a big sell-off of state-run enterprises.
But Zambian hopes for a bright future gradually turned to disillusionment as Chiluba began to abandon egalitarian principles and processes.
Tarnished image
Corruption became widespread at all levels and crime increased. The sell-off of the state copper mines was botched and many of the mines company's assets vanished into thin air.
In the meantime, the free-market economy failed to deliver and three quarters of Zambia's population continued to live in poverty.
What's more, Frederick Chiluba's personal image suffered badly when he appeared to be more interested in himself than his country.
Mwanawasa: Chiluba's successor brought charges of corruption against him
In 1996, he prevented former President Kaunda from standing against him in the presidential elections by changing the constitution to preclude candidates with parents born outside Zambia. Kaunda's father was from Zaire.
His hounding of Kaunda was not popular either at home or among the international community.
In 1997, he imprisoned the former leader for allegedly conspiring in a coup plot against him. Chiluba released him only after pressure from Africa's elder statesmen, Nelson Mandela and Julius Nyerere.
He also tried to strip Kaunda of his citizenship.
Then Chiluba tried to amend the constitution again to enable him to run for a third term and allegedly spent a lot of money bribing people to support his cause. Nevertheless, he failed and was forced to step down in 2002.
Corruption Charges
The following year, his hand-picked successor, Levy Mwanawasa, brought more than 100 charges of corruption against Frederick Chiluba including the theft of $35m of public funds allegedly funnelled into private bank accounts in London.
His wife Regina also faced charges of theft. Chiluba denied all charges, saying they were politically motivated. And he was acquitted after a six-year trial.
Corruption became widespread under Chiluba
However in 2007 he was found guilty of stealing $46m (£23m) of public money by a UK court.
To his credit, under Frederick Chiluba, freedom of speech in Zambia flourished and its media became as lively as anywhere in Africa.
Though he tried to extend his tenure in power, he did not resort to state-controlled oppression to get his way.
Internationally, he helped broker a peace agreement in neighbouring civil war-torn Democratic Republic of Congo.
Perhaps Frederick Chiluba's greatest legacy is that he established a lasting principle of democracy in Zambian politics.


Frederick Chiluba afariki dunia
Rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 68.
Bwana Chiluba amekuwa na ugonjwa moyo kwa miaka kadhaa.

Rais Chiluba aliiongoza Zambia kwa mwongo mzima katika miaka ya '90, na baada ya kustaafu alishtakiwa kwa sababu ya rushwa.
Frederick Chiluba alipata urais wa Zambia mwaka wa 1991, wakati Afrika inaanza kuingiia katika demokrasi ya vyama vingi.
Kabla ya hapo alikuwa kiongozi wa wafanyakazi.
Aliahidi kuleta mabadiliko lakini alipochukua uongozi Zambia ilikuwa imeshafilisika, naye aliacha rushwa kustawi.
Alipojaribu kujiongezea muhula wa tatu wa madaraka, alipingwa.
Pia alilaumiwa kuwa akipenda maisha ya anasa.
Baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2001, mrithi wake, Levy Mwanawasa, alimshtaki kwa shutuma za rushwa.
Baada ya kesi ya miaka 6 kuhusu ubadhirifu wa mali ya taifa, Frederick Chiluba aliambiwa hakuwa na makosa. .
Lakini katika kesi nyengine iliyofanywa katika mahakama makuu ya London, Chiluba alikutikana na hatia ya kuiba mamilioni ya dola ya fedha za serikali ya Zambia, kwa kutumia akaunti kwenye mabenki ya London. 
Chanzo: BBC



Monday, 6 June 2011

SHEREHE ZA KUWEKWA WAKFU NA KUSIMIKA ASKOFU- MBINGA

Kutoka kushoto kwenda kulia ni Mmliki wa Blog hii Friday Simbaya, Anold na Mpigapicha wa Rais Fred Maro muda mfupi kabla ya kuanza kwa Misa Takatifu ya kuwekwa na kusimika Askofu Mpya wa Jimbo la Mbinga, John Ndimbo katika Kanisa la Mt. kiliani.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu baada ya kumalizika kwa Misa ya kusimika Askofu wa Mbinga. Kulia kwake ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Kardinali Polycarp Pengo na kushoto kwake ni Askofu Mteule John Chrysostom Ndimbo.

 Rais Kikwete  wanne kutoka kulia akiwa Kanisa la Mt. Kiliani la Mbinga Jumapili wakati ya sherehe ya kuwekwa na kusimikwa Askofu wa Mbinga.


 
 Waamini mbalimbali wakifuatilia Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu na kusimika Askofu wa Mbinga katika Kanisa la Mt. Kiliani lililojaa pomoli hadi waamini wengine walikaa nje wakifuatilia misa kupitia Tv.



Waamini wakifuatilia Misa katika viwanja vya Emmanuel Square nje ya Kanisa kutokana na kukosa nafasi ndani na kukaa kwa nje wakifuatilia misa hiyo kwa kupitia Runinga mbili zenye vioo vikubwa.

DEDICATION OF NEW BISHOP OF MBINGA


By Friday Simbaya,
Mbinga
PRESIDENT Jakaya Kikwete has urged religious institutions in the country to provide more in vocational training centers so that more youths can get vocational skills and become self-reliance, hence increase self employment.
The president made the request on Sunday during the Episcopal Ordination of new Bishop of Mbinga, Rev. John C. Ndimbo of the Roman Catholic Diocese of Mbinga in Ruvuma Region.
He noted that religious institutions should invest more in the vocational training centers than anything else whereby youths especially dropouts can have the chance of getting vocational skills and help them become self reliant.
“We are asking for your favor  to build many vocational centers in the country so that help the government to make more people to become self esteemed and become self employed rather than them waiting for white collar jobs which are very limited and not sufficient enough for everyone, hence prepare them for the competitive labour market in the process,” he said.
He said that the government cannot afford to give job opportunities to everyone because there fewer job opportunities as compared to the number of people who  are in need in the country, but with advent of more  vocational training centers, it will help them become self reliance
.
Kikwete emphasized that people should develop the spirit self motivation and become hard workers and stop sitting around idle bickering and backbiting people around , if they want to attain the better life because  better is not  like manna dropping from heaven.
“People should utilize their time effectively but not just sitting around and complaining about hard life and backbiting people and playing gambling games but should instead get down to work, hence better life  and poverty reduction,” he added.
On the issue of drug trafficking, the president said that the business of drug is rampant in the country and war against it is becoming difficulty because it also involves people financial powers including religious leaders as while. He said that recently there was one bishop of the Catholic Church but he did not name him, who was intercepted by police in connection with drug trafficking.
He asked religious leaders in the country to help the government fighting the war against the illegal business of drugs because it is retarding  economic growth as it is killing youths are the future workforce due to drug abuse. However, he asked the church to help the government in reducing that kind of business by preaching to their followers about the bad thing of drugs abuse.

“We shall not leave any stone unturned but we shall reach for anyone involved in this kind of business” he pointed out.
 On the issue of the road, the president has promised the Mbinga residents that Mbinga Road will be completed before the end next year, through the support from American people. The Mbinga Road is will be constructed at a tarmac level and will reduce time spend on traveling because it will smooth no more dust and fast running vehicles from Songea to Mbinga will be brought.
He has also said after the completion of Mbinga Road, the government will focus on the road to Mbamba Bay which will be headquarters of Nyasa District. Adding if things go well with the donors will start construction of the road as soon as possible. But, it is not necessarily that we depend on donors to construct our roads we shall use own source funds to do that, he said.
On the issue of electricity, the president said Mbinga and the rest of Ruvuma Region, he said region will be connected to the national grid every soon. Mbinga and the rest of Ruvuma Region is currently using thermo-power stations for electricity.
In another development, President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), Rev. Yuda Tadeus Ruwaichi urged the government to make sure that it improves the lives of people by making a budget that going to meet people’s expectations and needs  during the forthcoming Budget Session in Dodoma, hence reduce the suffering of many people. Rev. Ruwaichi was accompanied by more than 25 bishops who are members of TEC and wished the country for prosperity, peace and tranquility during the celebration of 50th anniversary of independence of Tanzania this year.

The Mass of Ordination of the new bishop of Mbinga was driven by the Bishop of Dar es Salaam, Polycarp Cardinal Pengo. Other distinguished guests who attended the ceremony include the former President William Benjamin Mkapa and his wife Anna Mkapa, various Member of Parliaments for Mbinga Constituency and also regional and district leaders.







 
From left to right is the former First Lady, Anna Mkapa, Former President William Benjamin Mkapa, Bishop Polycarp Cardinal Pengo, new bishop of Mbinga, John Ndimbo, President Jakaya kikwete and President of Tanzania Episcopal Conference,  Bishop Yuda Ruwaichi in front of  St. Kilian Church of Mbinga, Ruvuma Region, at the ordination ceremony of new bishop of Mbinga on Sunday.




President Jakaya  kikwete was delivering his speech on Sunday during the ordination and dedication ceremony of new Bishop of Mbinga Diocese on Sunday.

Thursday, 2 June 2011

NEGLECTED TROPICAL DISEASES



Kaimu Mganga Mkuu (W) Halmashauri ya Wilaya Songea, Dr. Stephen Mhando  akizungumza na wanasemina wakati akifungua Kikao cha Mkoa cha Kutathmini na Kuratibu shughuli za magonjwa  yasiopewa kipaumbele (Neglected Tropical Diseases) cha siku tatu mkoani Ruvuma 2010-2011, kilichofanyika Peramiho LEO. Kushoto kwake ni Mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele mkoani Ruvuma, Dr. Ida Ngowi. Magonjwa hayo ni kama vile Kichocho cha kibofu na tumbo, Usubi , Minyoo ya tumbo (Soil worms), Matende na Mabusha na vikope (Trachoma). (PICHA: FRIDAY SIMBAYA)

Sunday, 22 May 2011

NO PLACE LIKE HOME

He is not dead! We have such people in many areas of the country who are sleeping near a dust bin at the bus stations. Indeed they have no place to call their home but they decide staying in such situation like this young man who was found yesterday get snoozing on the pavement in the open air in the presence of people at the Songea Town Main Bus Stand in Ruvuma Ruvuma. After they have done tiresome jobs as callboys and so on they call it day’s work. Some of them carrying parcel and luggage of travelers, who are traveling to and fro Ruvuma, they get rest just like that. Later on they get some food just right their at bus stand premises from the so called ‘Mama lishe’ or street food vendors nearby. Nevertheless, Songea Main Bus Station is facing the problem of filthy because everything is done under one roof, with uncollected garbage in many parts of the stand grounds. But what is the town fathers and municipal council authorities doing to correct the situation the bus stand and problem it is going through at moment hence reduce health hazards and prevent the epidemic contamination disease like Cholera? Prevention is better than cure.



 
Kina mama wauza dagaa wakisubiri wateja wakununua bidhaa hiyo kama walivyokutwa jana katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Dagaa hao kutoka Ziwa Nyasa katika Wilaya Mpya ya Nyasa, Jimbo la Mbinga Magharibi walikuwa wanauza kopo la lita moja kati ya Tshs. 1,500/- hadi 2,000/- na kisado cha lita nne kati ya shilingi 6,500/- hadi 7,000/-.



Tuesday, 17 May 2011

SEMINA KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU TZ

Katibu wa CWT Mkoa wa Ruvuma ambaye pia alikuwa ndiye Mratibu wa Mafunzo, Mwl. Luya Ngonyani akitoa mada wakati ya semina ya sera ya mafunzo na haki kwa viongozi wa CWT kutoka Kata Nne za Litisha, Maposeni, Peramiho na Lilambo wilayani Songea. Jumla ya washiriki wa semina hiyo ni 40. Semina hiyo ilifanyika leo Peramiho Shule ya Msingi, Songea Vijijini.

Washiriki wa semina ya sera ya mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi CWT na wawezeshaji muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina hiyo. walioketi kutoka kushoto kwenda kulia ni Mwl. Mwahija Luambano Mwakilishi wa Walimu Wanawake wilayani Songea, Mwl. Gervas Ngondo Mweka Hazina CWT, Mwl. Luya Ngonyani Katibu CWT Mkoa/ Mratibu wa Mafunzo, Mwl. Beno Mwenda Mwenyekiti CWT Wilaya na Mwl. Manyula M. Nkomolla Katibu CWT Songea Vijijini.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KATIKA KUMSIMIKA ASKOFU NDIMBO

ASKOFU MTEULE WA JIMBO LA MBINGA
MHASHAMU JOHN C. NDIMBO





RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kumsimika Askofu Mpya wa Pili wa Jimbo Katoliki la Mbinga mkoani Ruvuma hapo tarehe 05.06.2011. Aidha, Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu huyo itaongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Da es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Akiongea na Blog ya http://www.fridaysimbaya.blogspot.com/ leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Jimbo la Mbinga Pd. Jospeh Mwingira amesema kuwa Rais Kikwete ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kumsimika rasmi na kuweka wakfu Askofu Mteule wa Jimbo la Mbinga, Mhashamu John Chrisostom Ndimbo.

Jimbo Katoliki la Mbinga limepata Askofu Mpya aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Pili wa Jimbo hilo. Mwashamu Askofu John Ndimbo aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Askofu wa pili wa Jimbo Katoliki la Mbinga hapo tarehe 12 Machi, 2011.
Uteuzi huo umefuatia kustaafu kisheria kwa Mhashamu Askofu Emmanuel Mapunda aliyeliongoza jimbo hilo kwa miaka 21 mpaka sasa. Mhashamu Askofu Emmanuel Mapunda amefikisha umri wa miaka 75 ambayo kwa taratibu na sheria za Kanisa Katoliki, maaskofu wake wafikapo umri huo wanapaswa kustaafu majukumu ya kuliongoza jimbo.

Askofu Mapunda alifikisha umri huo tarehe 10. 12. 2010. Baada ya kupeleka maombi ya kustaafu kwa mkubwa wake Papa Benedikto XVI, Askofu huyo alikubaliwa na kuomba aendelee kusimamia Jimbo la Mbinga hadi hapo Askofu mpya atakapoteuliwa.
Askofu Jonh C. Ndimbo alizaliwa tarehe 12. 10. 1960 huko Kipololo katika Parokia ya Lundamato Jimbo la Mbinga. Wazazi wake walikuwa Chrisostom Ndimbo na Fransiska Ndunguru. Ubatizo alipata tarehe 13.11 1960 na kipaimara tarhe 29.10. 1972.

Shule ya msingi alisomo huko Kipololo katika Porakia ya Lundamato la Jimbo la Mbinga, kwa darasa la kwanza hadi nne mwaka 1969 hadi 1972. Masomo ya darasa la tano hadi saba alisoma huko Hanga Seminari katika Jimbo Kuu la Songea kuanzia mwaka 1973 hadi 1975.

Masomo ya sekondari alisoma katika Seminari za Likonde katika Jimbo la Mbinga (wakati huo lilikuwa Jimbo la Songea) na Nyegezi katika Jimbo la Mwanza. Kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1976 hadi 1979 huko Likonde. Kidato cha tano hadi cha sita mwaka 1980 hadi 1981 huko Nyegezi.

Pia alipata mafunzo ya kijeshi huko Urujoro-Arusha maka 1982. Kisha aliendelea na malezi na kozi ya upadre katika Seminari Kuu Peramiho. Falsafa alisoma mwaka 1983 hadi 1985 na teolojia mwaka 1986 mpaka 1989. Alipewa Daraja Takatifu la Ushemasi Juni 1988 na upadre 21.06. 1989 huko Mbinga na Mhashamu Askofu Emmanuel A. Mapunda wa Jimbo la Mbinga. Yeye ni miongoni mwa mapadre sita (6) waliopadrishwa mwaka huo jimboni Mbinga.

Baada ya upadrisho Pd. John Ndimbo alitumwa seminari ya Likonde kuwa mwalimu na mlezi wa waseminari. Mwaka 1990 alipelekwa Ufilipino kwa masomo ya juu ambako alipata shahada ya kwanza na ya pili katika masomo ya sayansi na utawala wa elimu. Vyuo alivyosoma ni Rigina Carm Katikaeli kilichopo katika jiji la Manila na cha DE LA SALLE hapa hapo Manila. Alihitimu masomo hayo mwaka 1994 na kurudi jimboni Mbinga.

Tarehe 8 Septemba 1994 aliteuliwa na Mhashamu Askofu Emmanuel Mapunda kuwa Gombera wa seminari Likonde wadhifa aliodumu nao mpaka tarehe 28. 09.2010 alipoacha kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu ya Baraza la Maaskofu Tanzania tarehe 3 Agosti 2010.

Mhashamu Askofu John Ndimbo ni Askofu pacha wa Mhashamu Askofu Bernadine Mfumbusa wa Jimbo Katoliki la Kondoa katika Mkoa wa Dodoma. Kwani, siku alipoteuliwa na kutangazwa Askofu John Ndimbo wa Jimbo la Mbinga, tarehe 12 Machi, 2010, Baba Mtakatifu Benedikto XVI alianzisha Jimbo la jipya la Kondoa lililozaliwa kutoka Jimbo la Katoliki la Dodoma. Kisha akamteua Pd. Bernadine Mfumbusa, ambaye alikuwa makamu  mkuu wa taaluma katika chuo kikuu cha Kanisa Katoliki cha Mt. Augustino (SAUTI) Mwanza .

“Jimbo jipya la Kondoa lina eneo la kilometa za mraba 13, 210, watu 541,345, wakatoliki 46,067, mapadre 17, watawa 87. kumbe, Jimbo Katoliki la Mbinga ambalo lina milikiwa na Mhashamu Askofu John Ndimbo lina eneo la kilometa za mraba 11, 400, watu 532,019, wakatoliki 418,000, mapadre 69 na watawa 270,” sehemu ya taarifa inaelezea.

Uteuzi wa maaskofu hawa umepokelewa na wakristo na Watanzaia kwa ujumla kwa hisia za pekee na tofauti. Kundi kubwa la watu linasifu na kupongeza uteuzi wao, lakini wengine wanaonja kwa karibu sana pengo waliloacha katika nafasi zao walizoziacaha. Wote hao wamekuwa katika nafasi za juu na nyeti za kitaaluma katika Kanisa letu.

Mhashamu John Ndimbo alikuwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu TEC baada ya kushughulika na taaluma kwa miaka 22 katika seminari Likonde, hivyo kwa uhakika ana mang’amuzi na uzoefu wakutosha.

Mhashamu Askofu Mfumbusa amekuwa makamu wa mkuu wa taaluma katika chuo cha SAUTI-Mwanza na mhadhiri nguri wanafunzi wa kozi ya uandshi wa habari. Hapo alikuwa mhimili mkubwa wa taaluma ya mwasiliano.

Wahashamu maaskofu Benedine Mfumbusa na John Ndimbo walikula kiapo cha utii na kukiri kanuni ya Imani kwa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki Papa Benedikto XVI huko Roma katika Kikanisa cha mweyeheri Kardinali Henry Newman hapo tarehe 4 Aprili, 2011. Katika nafasi hiyo walikabidhiwa vitendea kazi vya kiaskofu.

"Tunawatakia maaskofu wetu hawa amani, baraka na nguvu katika wajibu huo mpya. Mungu aandamane nao daima."



WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...