Thursday, 16 September 2010

MTEMVU AWAONDOLEA WASIWASI WANANCHI

MGOMBEA kiti cha Ubunge Jimbo la Temeke kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abasi Zuberi Mtemvu amewatoa wasiwasi wapangaji wa nyumba za kota zilizopo Temeke mwisho kwa kuwaeleza kuwa zoezi la kuvunjwa kwa nyumba hizo sasa limesitishwa.

Mgombea huyo alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi uliyofanyika katika uwanja wa MjiMpya Kata ya Azimio jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati wa watu.

Akifafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo Mtemvu alisema serikali iliyoko madarakani imejipanga kujenga majengo ya ghorofa katika eneo hilo ambapo ujenzi wake ukikamilika wapangaji wa awali wa kota watapewa umuhimu wa kwanza kufikiriwa katika kupanga kwenye maghorofa hayo.

Alisema si vyema kuanza zoezi la uvunjaji wa kota hizo bila kuzingatia usalama wa wananchi na mali zao katika kipindi cha mpango huo.

Kota hizo zilizopo eneo la Temeke mwisho zilijengwa miaka mingi iliyopita katika mfumo wa familia moja, mbili na tatu hata hivyo nyumba hizo zimeanza kuchoka na hata baadhi yake kuanza kuharibika.

Kwa upande mwingine mgombea huyo aliwataka wanawake wa jimbo hilo kujiunga pamoja na kuunda vikundi vidogo vidogo (VICOBA) ili waweze kupata misaada ya uwendelezaji wa vikundi vyao ili kuondokana na umasikini wa kipato na kuboresha familia zao.

Akizumgumzia huduma za jamii upande wa elimu alisema endapo atachaguliwa tena kuongoza jimbo hilo atahakikisha kuwa kata ya Azimio inapata sekondari ya kidato cha tana na sita.

Wednesday, 15 September 2010

ABASI MTEMVU


Bw. Abasi Zuberi Mtemvu Mgombea Mbunge katika Jimbo la Temeke kupitia tiketi ya CCM (mwenye mkono juu na vazi ya kijani la CCM katikati) akilakiwa na wanacchama na wananchi katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi 2010 uliyofanuika Kata ya Azimio jijini Dar es Salaam.

MWANDISHI AVAA KHANGA YA CCM NA BAADAYE KUPANDA GARI LA MATANGAZO YA CHAMA HICHO NA KUTOKOMEA NALO----HABARI NDIYO HIYO!








Mwandishi wa habari ambaye akufahamika jina lake mara moja amekutwa akiwa amevaa Khanga ya Chama Cha Mapindizi (CCM) katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 uliyokuwa unahutubiwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Temeke, Bw. Abasi Zuberi Mtemvu leo. Mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa MjiMpya-Tawi la Kichangani (CCM) Kata ya Azimio Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Tuesday, 14 September 2010

MAMBO YA PWANI


Wachuuzi wa samaki wakimuandaa samaki aina ya pweza katika soko la samaki Magogoni jijini Dar.

Residents of Dar es Salaam were enjoying a ride on the MV Magogoni in the Indian Ocean during the weekend going to Kigamboni.

USAILI WAANDISHI MATUMBO JOTO

Waandishi wa habari wakijisomea vijarida mbalimbali katika Ofisi ya Waandishi Mazingira (JET) jijini Dar es Salaam walipokuwa wakisubiri kuingia kwnye usaili ofisi hapa kwa ajili ya 'Exchange Programme' katika nchi za Ethiopia, Kenya, Uganda na Malawi jana.

MVULANA MPIKA VITUMBUA

UGUMU wa maisha na umaskini wa wazazi wa Adam Mussa (18) wampelekea kuwa mjasliamali wa kupika vitumbua Barabara ya Kawawa Kituo cha Moroco jijini Dar es Salaam.

ADHA YA USAFIRI DAR

ADHA  ya usafiri Dar es Salaam wanafunzi hawathaminiwi hii ilidhihirika jana katika Kituo cha daladala Mtoni Mtongani ambapo mwanafunzi huyu katika picha (watatu kutoka kulia) akionekana kushangaa wakati watu wazima wakigombea usafiri.

Sunday, 12 September 2010

ABOOD BUS SERVICE

Mafundi na abiria wa bus la Abood akisaidiana kutengenaza ekizoti paipi ya bus baada kukatika katika eneo la Igemi katikati ya Mahenge na Mtandika Wilaya ya Killolo mkoani Iringa jana majira ya saa 3 asubuhi. Bus la Abood lilianza safari kutoka Iringa Mjini kwenda Dar saa 1 asubuhi lakini lilipofika eneo la Igemi 'exhust pipe' ilichomoka na mafundi wa basi wakatengeza kidogo ndipo tulipofika Hoteli ya Aljazeera walilichomelea na tukaenedelea safari hadi Ubungo saa 9:30 hivi.

Foleni ya magari kama ilvyokutwa katika eneo la Igemi katika ya Mahenge na Mtandika wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa ya kisubiri kuruhusiwa na watengezaji wa barabara ya Tanzam.

Friday, 10 September 2010

EID AL-FITR IS SUBJECTED TO THE SIGHTING OF THE MOON


Eid al-Fitr falls on the first day of Shawwal, the month which follows Ramadan in the Islamic calendar. It is a time to give in charity to those in need, and celebrate with family and friends the completion of a month of blessings and joy.

At the end of Ramadan, Muslims throughout the world have a joyous three-day celebration called Eid al-Fitr (the Festival of Fast-Breaking).

Eid Al-Fitr is a holiday marking the end of Ramadan, the month of fasting which is one of the greatest religious observances in Islam.

Nawatakia Eid al -fitr njema wasomaji wote yangu wa blog.

TOO MUCH OF EVERYTHING IS DANGEROUS

Mambo ya Eid al-fitr yalivyokuwa Mjini Iringa leo. An identified man was caught sleeping after he over celebrated Eid al-Fitr near VIP Pub in Iringa Municipality, Iringa Region.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...